Maofisa wa Kyrgyz wanasema kuwa wafungwa hao waliamua kushona midomo yao baada ya wakuu wa magereza kuwalazimisha kula ili kuvunja mgomo wa kutokula waliouanza tangu Januari 17, 2012.
Kitendo cha kuwalazimisha kula kilisababisha ghasia baina ya wafungwa na askari ambapo inaripotiwa mfungwa mmoja alifariki dunia na wengine kujeruhiwa kiasi cha kupelekwa hospitali kwa matibabu.
Kyrgyzstan ilijipatia uhuru wake mwaka 1991 kutoka kwa Muungano wa nchi za Kisovieti uliovunjika.
Inaripotiwa pia kuwa hali katika magereza ya nchi hiyo ya Bara la Asia ya Kati ni mbaya.





RSS Feed