UPDATE: Post hii imejaa audio na inakuwa nzito kufunguka, hivyo kila inapotokea taarifa mpya, nitaianzishia post yake ili kupunguza usumbufu wa "loading time".

Siku ya leo, taarifa na habari kuhusu mgogoro wa Madaktari na Serikali Tanzania zitaongezwa hapa kama "updates" au "mpya" kadiri zitakavyopatikana kutoka kwenye vyanzo mbalimbali vya habari. 

Hivyo usikose kurejea chapisho hili (post) mara kwa mara kuona ikiwa imeongezwa habari mpya.
Taarifa Habari TBC saa 12 asubuhi

Taarifa Habari Saa moja asubuhi

Jicho la Ng'ombe Clouds FM

Taarifa Habari Clouds FM saa moja asubuhi
Clouds FM mapitio ya magazetini

Spika akifungua bunge na kutoa taarifa fupi kuhusu Mgomo wa Madaktari

Kazi ya kwanza aliyoifanya Spika Anne Makinda leo asubuhi ni kuelezea maendeleo ya hatua zinazochukuliwa kumalizia mgogoro wa madaktari.

Alisema Kamati ya Bunge ilimaliza kazi na jana usiku walikutana na kamati ya uongozi na baadaye Spika alizungumza na Waziri Mkuu na Rais Kikwete na wakakubaliana jambo.

Alisema jambo hilo litawekwa wazi mchana huu. Hata hivyo alisema kwamba Waziri Mkuu anaendelea na juhudi za kukutana na wahusika.

Walichoomba wabunge kupitia Spika ni madaktari kurejea katika kazi zao na kuendelea kuzifanya.

Alsiema waliosaabbisha mawasiliano mabaya watachukuliwa hatua na madai yao ya dharura kushughulikiwa.

Alisema wajumbe wa Kamati walihuzunishwa sana na hali iliyopo katika hospitali ya Muhimbili na katika hali hiyo Spika alisema si jambo la kuzungumza kwa ushabiki kwani ni jambo kubwa.

via blogu ya Lukwangule 

Madaktari wameitikikia wito wa Waziri Mkuu na kufika kwenye ukumbiwa CPL Muhimbili

 


Comments




Leave a Reply