*Kwenye video ya pili, dakika ya 52, yupo mtoto wa afisa polisi anayetoa maneno ya uchungu mkubwa. Usikose!

Hivi ni video zinazoonesha jinsi biashara ya mihadarati ilivyo na mtandao mkubwa.

Biashara ambayo hata wewe usipokuwa makini unaweza kujikuta umehusika.

Video inayotanabahisha maafisa wapelelezi wanavyoweza kuwa washiriki wakuu wa biashara hiyo, ama kwa kutaka au kwa shuruti, na jinsi ilivyo vigumu kutenganisha aliye mkweli na mwongo. 

Lipo tukio la kutisha kwa jinsi ambavyo askari polisi aliyepewa jukumu la kuhifadhi ufunguo uliokuwa wa sehemu ilikokoifadhiwa shehena ya mihadarati aina ya "cocaine", alivyouawa kinyama kwa kupigwa jumla ya risasi 22, ikipenya moja baada ya nyingine kwa takriban daika 15 katika sehemu mbalimbali za mwili wake, katika boma lake huku wanawe wawili wadogo, wakike na wa kiume wakishuhudia, ambapo mmoja anahadithia alichokiona.

Video hii pia inaonesha jinsi watu waliopewa ajira ya kusafirisha bidhaa, walivyojikuta na wazo la kutaka kujua walichokuwa wakisafirisha mara kwa mara, ndipo walipofungua na kutambua ilikuwa ni mihadarati.

Utaona vile vile jinsi ilivyo rahisi kwa askari na watumishi wazuia magendo wenye tamaa, ilivyo rahisi kujihusisha na biashara hiyo na kuwatisha askari na watumishi waaminifu wanaofanya kazi kuzuia mihadarati. Magari ya serikali na 'ambulance' zaweza kutumika kwa shughuli hii, jambo ambalo uongozi mkubwa unahusika kwani haiwezekani magari hayo kutumika bila ruhusa, ufahamu na notisi ya viongozi wa jeshi husika.

Vile vile utaona jinsi ilivyo rahisi kwa watu waroho wa utajiri wa haraka wanavyoweza kujichomeka kwa nguvu katika mihadarati iliyokamatwa, ili tu wapate kiasi cha mihadarati hiyo kwa ajili ya kujipatia fedha.

Mohammed Ali na kikosi cha wanahabari wadadisi wanaelezea matokeo ya uchunguzi wao.

 


Comments

Jaramba
02/02/2012 08:48

This is very touching Subi

Reply
02/02/2012 08:58

I agree @Jaramba.
I've been watching videos by Mohamed Ali & team, and wished we had more of him and the likes of Jerry Muro in Tanzania, perhaps the society would have been more informed.

Reply



Leave a Reply