Yaliyomo
Kutabaruku............................... 7
Salamu za Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania ...................... 9
Shukrani.................................. 11
Dibaji....................................... 15
Utangulizi................................. 17
Vifupisho................................. 23
Sehemu ya Kwanza
TANZANIA TULIKOTOKA
1. UKOLONI TANZANIA BARA.... 27
2. HARAKATI ZA UKOMBOZI...... 39
3. UHURU................................... 47
4. MAISHA BAADA YA UHURU... 57
Sehemu ya Pili
TANZANIA TULIPO
5. JUBILEI YA MIAKA 50 YA UHURU WA TANZANIA BARA.............. 69
6. JUBILEI NI KUANGALIA TUNU ZETU KAMA WATANZANIA..... 78
7. JUBILEI NA CHANGAMOTO ZETU....................................... 86
Sehemu ya Tatu
TANZANIA TUNAKOKWENDA
8. JUBILEI NI KUANZA UPYA....107
9. KANUNI YA TIBA MCHEPUO KWA MAENDELEO YA TAIFA LETU....................................... 133
TATHMINI NA MOTISHA........ 145
HITIMISHO............................. 159
REJEA..................................... 169
MUHTASARI:
Kitabu hiki kimegawanyika katika sehemu kuu tatu. Sehemu ya kwanza ni Tanzania - tulikotoka ambayo inaongelea masuala ya ukoloni, harakati za ukombozi, uhuru na maisha baada ya uhuru. Sehemu ya pili inaongelea Tanzania – tulipo inayozungumzia hali yetu leo kiuchumi, kisiasa na kijamii nikijadili changamoto zetu kama taifa na tunu zetu tulizonazo tangu uhuru mpaka sasa kama Watanzania na maana na umuhimu wa sherehe zetu za Jubilei ya miaka 50. Hatimaye, sehemu ya tatu, inazungumzia Tanzania – tunakokwenda (mwanzo mpya) ikijadili wapi tunakokwenda kama taifa yaani kuwa na mwanzo mpya na kuingalia kanuni ya tiba mchepuo kama nyenzo ya kutufikisha huko. Kama yule mshairi na mtunzi wa vitabu wa Uingereza Robert Louis Stevenson alivyopata kusema kwamba, “Usipime siku yako kwa yale uliyovuna bali pima kwa yale uliyopanda.” Malengo hayo ndiyo yamenifanya nipande mbegu ya kitabu hiki kwa kuitakia mema nchi yangu kwa miaka 50 mingine.
Mwisho natabaruku kitabu hiki ni kwa heshima ya taifa langu Tanzania linalofanya Jubilei ya miaka 50 ya uhuru wake na kwa namna ya pekee Mama yangu mpendwa Christina Shija, baba yangu mpendwa marehemu Gabriel Kasembo, marehemu babu yangu Chifu Yohana Kilangabhana Kasembo, marehemu bibi yangu Agatha Mija Michael, Hayati Askofu Mkuu Anthony Mayala, Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na Watanzania wote ninaochangia nao utaifa na nia njema ya kuitakia mema nchi yetu na zaidi wenye moyo wa dhati wa kujenga taifa la Tanzania lenye heshima, upendo, amani na maendeleo ya kweli na ya uhakika kwa kizazi hiki na kijacho! Nakutakieni usomaji mwema na mafanikio tele katika maadhimisho ya jubilei ya miaka 50 ya uhuru wa Tanzania huku tu tukifakari uwepo, maisha na mustakabali wa taifa letu !
KWA KUAGIZA NAKALA YA KITABU HIKI ADIMU NA ADHIMU KWA TAIFA LETU, WASILIANA NA:
JOHN MTWALE KASEMBO
P.O BOX 22, PERAMIHO.
SIMU: 0755 417 074 / 0712 120 775
BARUA PEPE: jmkasembo02@yahoo.com
Alisoma shule ya msingi Shamaliwa na baadaye masomo ya Sekondari kwenye Seminari za Nyegezi - Mwanza na Maua - Moshi.
Ni mwezeshaji na mtoa mada wa mambo ya uongozi, dini, vijana, falsafa, ujasiriamali na amali za maisha. Ni mhitimu wa masomo ya falsafa na dini katika Chuo cha Mtakatifu Augustino Peramiho ambacho ni Chuo Kishiriki cha Chuo Kikuu cha Urbana, Roma.
Pia. yeye ni mtafiti wa maendeleo ya Tanzania. Sasa anaendelea na masomo ya Shahada ya Kwanza ya Teolojia katika Chuo hicho hicho.
Kitabu hiki kimechapishwa na kampuni ya Kolbe printing press, Nairobi nchini Kenya.


RSS Feed