Yafutayao ni maoni ya Mashingo aliyoyatoa katika chapisho lenye kichwa cha habari, "Je wajua: Kwenda kutibiwa India inawezeka ni "biashara" ya watu fulani?"

1. tatizo la watanzania walio wengi ni kufuata mkumbo bila kutumia angalau dakika kadhaa kufikiri. kwa nini India? kwani hakuna nchi nyingine ya afrika ambayo ina huduma bora zaidi? sasa hivi mpaka internet wameanza kutangaza hospitali maalum kwa ajili ya watanzania. hamjiulizi mbona wahindi tulio nao hapa hawarudi kwao?

ni ukweli kwamba ukireffer mgonjwa kuna commission. nikiwa kama mmoja wa waliopata 'bahati' ya kusindikiza wagonjwa India, niliahidiwa 

kupewa sponsorship na 'wenyeji wetu' iwapo ningefacilitate more refferals. Hawajifichi,hawa ni wafanya biashara sio ndugu zetu,so i don't blame them.Iits our own stupidity.

kwenda kutibiwa nje sio kosa au dhambi. Lakini iwe kweli imeshindikana hapa kwanza. Sio hali ilivyo hivi sasa ambapo viongozi wa juu wana haki ya kwenda 'KUCHEKIWA AFYA' nje ya nchi wao na familia zao. Amiin nawaambia, kama hili halitapigiwa kelele na kufutwa,hali ya hospitali zetu hasa hizi ambazo ndio wengi wetu tunakwenda itazidi kuwa hovyo. Umeona wapi mtu akahangaika kuboresha nyumba asimolala! Hivi tunaonekanaje huko nje?

2. Sikatai kweli kuna vitu wametuzidi, lakini tungeweza kuvifanya hapa kwetu kama tukiamua. Na serikali zinazojali na kufanya kazi kwa kutumia akili na kuona mbali huwa unaleta wataalam au unapeleka wa kwako huko unakodhani wamekuzidi kimaarifa ili watu wajifunze sio kupeleka wagonjwa. Mbona kenya walikuja kujifunza tunaendeshaje Mfumo wetu wa bima ya afya.

3. Kingine ni kuingiliwa kwa fani ya utabibu. Leo hii Tanzania kila anayejisikia kujiita daktari anajiita tu na bila kujali uwezo wake anatibu watu. Sijui kama Watanzainia hata wanajua kutofautisha. Na hii matokeo yake ni kugeneralise kuwa hii fani ni ya wasanii. Ni nchi pekee ambayo mgonjwa akifika kwa daktari anamkabidhi kila kitu na kumuachia afanye maamuzi yake,bila hata kuulizia matokeo yatakua yapi. Ni wagonjwa wangapi huwa hata wanauliza aelezwe anachoumwa na wajadili njia za matibabu na pengine kukataa njia moja na kuchagua nyingine! Ni wangapi wamefanyiwa upasuaji bila hata kuuliza kama ndio njia pekee,au hata kujua kwa juu juu tu kinachoenda kurekebishwa au kutolewa? Na hili ni tatizo,kwani hata mgonjwa anapoelezwa tatizo lake na options za matibabu wengi huwa wanaona kama wapotezewa muda.

Haya,with all due respect, hawa madaktari wanajeshi wanaopelekwa muhimbili wanatokea wapi? huko walikokua walikua wanareffer wagonjwa muhimbili kwa madaktari bingwa, sasa leo aliyekushindwa Lugalo ndio unamkuta muhimbili kitengo ambacho hata walio muhimbili kwenyewe sio wote wana utaalam nako. Ni kweli mtu yeyote anaweza akaitwa kutoka alikokuwa (jeshini, wizarani, mstaafu) na akaziba pengo! Sitaki kuamini kwamba ni rahisi hivyo. Na sidhani kama ni lazima sana wavae magwanda,ni wanajishi sawa, lakini pale ni hospitali,kuna maadili yake. Hata hospitali za jeshi huvai magwanda unapokua unatoa huduma. Au hawataonekana kuwa ndio waliopelekwa na serikali?

4. Dharau kwa vituo vyetu vya afya. Ni kiongozi gani alishawahi kwenda kwa mfano mwananyamala,au hata Muhimbili kwenyewe akapigwa picha akiwa kwenye foleni ya kusubiri tiba? lakini ni wangapi walipiga picha kwa babu wakinywa kikombe ambacho hata tafiti zake zimefanyika baada ya watu mamia kuwa wameshakunywa? na waziri wa ujenzi, Mh magufuli akatangaza kutenga tsh billioni 10 kwa ajili ya kumjengea barabara ili mkwanywe vizuri? ile ilipangwa kwenye bajeti? kama waliweza kumtengenezea mazingira mazuri ili mkanywe msichokijua,kwa nini wasifanye hivyo huku ambako wengi tayari angalau mna ufahamu nako na hata wasio na imani wanapona? 

Ili kupitisha dawa mpya inabidi ifanyiwe utafiti si chini ya miaka 10! hii ni kwa sababu kila dawa ina madhara ya muda mfupi na yale ya muda mrefu. Leo hii wangapi wamejitokeza kuelezea madhara yaliyowakuta baada ya kunywa kile kikombe? Ni kweli hakuna,au ndio kila mtu na mzigo wake kwa sababu ulienda mwenyewe?

Mwisho kabisa, ningependa kutoa mifano michache. 

Iwapo umelipia kampuni ya ulinzi ikuletee mlinzi,unatarajia mlinzi nyumbani kwako kama mlivyokubaliana. pale mlinzi asipotokea, utakachofanya ni kwenda kwa meneja au mwenye kampuni kudai mlinzi kama mlivyokubaliana. 

Timu yetu ya taifa hatupangi sisi watazamaji. Tunakabidhi majukumu yote kwa kocha na kamati yetu ya ushindi. Na kama haikutuletea matokeo mazuri, tutalaumu mchezaji fulani lakini anaebeba lawama zote na kuwajibishwa ni kocha kwa kuchagua watu ambao hawakutufikisha pale tulipotaka.

Sasa kwa nini Watanzania tunaoteseka hatujaiuliza wizara na serikali kwa nini haiwawajibishi hawa watabibu ambao hawatoi huduma wanayotakiwa kuitoa?
 


Comments




Leave a Reply