Baadaya ya kuwakataza waumini wake kujamiiana siku za kazi, Mchungaji wa Kanisa la Ufufuo Mtaa wa Ituha kata ya Ilomba, mkoani Mbeya; uongozi wa Serikali ya Mtaa huo umesimamisha huduma hiyo kutokana na kuhatarisha mahusiano ya ndoa.

Afisa mtendaji wa mtaa huo Pius Moses amemtaja mchungaji huyo kuwa ni John Leonard na kusema kupitia mafundisho yake amekuwa akiwakataza waumini wanandoa kukutana kimwili na pia kutohudhuria misiba akisema dhehebu hilo haliamini kifo.

Afisa huyo amesema pia mchungaji Leonard anatuhumiwa kuwakataza waumini wake kusalimia na watu wengine kwa kupeana mikono kutokana na kile kinachoaminiwa na kanisa hilo kuwa muumini wa dhehebu jingine ni mfu.

Mmoja wa waaumini wa dini hiyo aliyejitambulisha kwa jina la Mama Pendo amekiri mchungaji wake kuwashinikiza wanandoa kutokutana kimwili siku za katikati ya wiki isipokuwa siku ya jumapili pekee kwakuwa ndiyo siku ambayo Mungu alipumzika.

Jitihada za kuzungumza na mchungaji Leonard zimegonga mwamba kufuatia kuhamia kusikojulikana tangu Februari mosi kabla ya siku aliyopangiwa na serikali ya mtaa kuhama.

Taarifa imeandikwa na Joachim Nyambo, via blogu ya RumAfrica
 


Comments

AM
11/02/2012 13:01

Wachunganji hawa ni upuuzi mtupu. Wanajitakia ajira na kuwaondoa akili (brainwash) wananchi!

Reply



Leave a Reply