Nimepokea utenzi ufuatao kwenye email, simfahamu mtunzi, ila shukrani zote zimfikie.
Rais hakika naona aibu,
Sijui wewe una sababu,
Umerudi uwe karibu,
Huku madakitari wagoma.

Rais umefika jana tu,
Leo kutwa na viatu,
Fungua benki ya watu,
Huku madakitari wagoma.

Rais nami umenchosha,
Watu pia umewachosha,
Sio siri hii inajionesha,
Huku madakitari wagoma.

Rais basi nenda Amana,
Muhimbili napo umeona,
Wagonjwa kila kona,
Huku madakitari wagoma.

Rais Bungeni Dodoma,
Wanakula wao nyama,
Muhimbili kumesimama,
Huku madakitari wagoma.

Rais hili tia makini,
Sio za huku mijini,
Hospitali za kijijini,
Huku madakitari wagoma.

Rais leo madakitari,
Kesho pengine askari,
Walimu nao wasubiri,
Huku madakitari wagoma.

Rais kemea hata hili,
Achana na EPA na dili,
Hayo sie tutasubili,
Huku madakitari wagoma.

Rais huko muhimbili,
Wakudanganya ni shwali,
Hakuna hata moja faili,
Huku madakitari wagoma.

Rais sema hata neno,
Watanzania tuone upo,
Kemea huyu we pepo,
Huku madakitari wagoma.

Naandika ushairi huu huku chozi linalengalenga, nilipita sehemu leo kuna mtu 1 alikuwa anaelezea ana mgonjwa Muhimbili mahututi anataabika toka mgomo uanza anakunywa pain killer. Rais amerudi ameishia enda kufungua FnB bank. Uwiiiii Mungu tusaidie sisi tusiojisaidia wenyewe pengine twaweza ona hata mwanga.

Mungu ibariki Tanzania.
 


Comments

hobidan
04/02/2012 17:27

kweli hilo shairi hili sio mchezo,mimi kusoma tu machozi yamenitoka.

Reply
Baba T
06/02/2012 08:50

Kwakweli inasikitisha sana, ila huenda malipo ni hapahapa, tutaona

Reply



Leave a Reply