Akijibu swali la Mbunge wa Mbeya mjini Joseph Mbilinyi, aliyetaka kujua Tanzania inanufaika vipi na uwekezaji wa kanali Muammar Gaddafi kibiashara, na kwa kuwa Tanzania haitambui serikali ya mpito ya Libya ni nani anayesimamia uwekezaji wa kibiashara wa marehemu kanali Muammar Gaddafi; Waziri wa nchi ofisi ya Waziri Mkuu, Uwekezaji na Uwezeshaji, Mary Nagu amesema kumbukumbu za kituo za uwekezaji zinaonyesha mradi mmoja tu ulioandikishwa kutoka nchini Libya na kampuni ya NORTH AFRICA INVESTMENT TRADING COMMPANY na si wa marehemu Qaddafi.
Akasema kampuni hiyo imeandika andiko la kibiashara la kuwekeza jumla ya dola za kimarekani milioni 5.8 na kutengeneza nafasi za ajira 160 pale ilipoinunua hoteli ya Bahari Beach iliyopo jijini Dar es Salaam.
source


RSS Feed