WAZIRI wa Mambo ya Ndani Shamsi Vuai Nahodha amekumbana na zahama ya kuzomewa kutoka kwa kundi la watu wanaodaiwa kuwa ni wafuasi wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) alipofanya ziara yake kichama katika mji mdogo wa Tunduma mkoani Mbeya.

Zomea zomea hiyo iliibuka mara msafara wa Waziri Nahodha ulipofika eneo maarufu la biashara kwa vijana wanaobadilisha fedha za kigeni ambapo kundi la vijana waliosimama pande mbili za barabara kuu iendayo Sumbawanga walianza kupiga mayowe na kuuzomea msafara huo.

Sauti za vijana haozilisikika zikihanikiza hewani zikisema, ‘aache kutumia rasilimali zaserikali kwa shughuli za CCM..hilo ni jasho la walipa kodi’

Wakati kundi hilo la vijana likizomea mmoja wa vijana ambaye hakutambulika jina lake alijikutakatika wakati mgumu wa kuwekwa chini ya ulinzi wa polisi na vijana wa Green Guard kwa madai kuwa wakati akizomea alikuwa akitaka kurushia mawe msafara huo.

Kijana huyo ambaye hakuweza kupatikana jina lake alichezea mkong’oto kutoka kwa vijana Green Guard na askari ambao walijichanganya katika kundi la vijana wa CHADEMA ambao walikuwa wakipeperusha bendera za chama chao.

Akizungumza wakatia kimkaribisha Waziri Nahodha ambaye pia ni mjumbe wa Halmashauri kuu ya TaifaCCM, Mwenyekiti wa CCM kata ya Tunduma Bw. Daniel Mwashiuya alisema kuwa kuna kundi la watu wachache ambao wamejipanga kuvuruga amani katika mji huo kwa kisingizio cha siasa.

Bw. Mwashiuya alisema kuwa CCM iko imara katika kukabiliana na vurugu hizo ambazo zinatishia amani na utulivu wa watu na mali zao.

Akizungumza katika mkutano wa hadhara uliohudhuriwa na kundi la wanachama wa CCM, Bw. Nahodha alisema kuwa amejionea mwenyewe hali ya uvunjifu wa amani na kwamba kwa kuwa yeye ndiye Waziri mwenye dhamana ya ulinzi wa wananchi na mali zao hawezi kufumbia macho ambapo alimuagiza Kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya kushughuliki ahali hiyo ikiwa ni pamoja na kupiga marufuku biashara haramu eneo hilo.

Tukio la aina hii katika eneo hilo ni la tatu ambapo tukio la kwanza lilikuwa ni wakati wa mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2009 uliolazimika kubadilisha njia wakati yalipotoke  amauaji ya mfanyabiashara wa mjini Tunduma ambapo mtu wa tatu kukutana na zahama ya kuzomewa alikuwa ni mke wa Rais Mama Salma Kikwete ambaye alikuwa katika ziara ya kampeni za uchaguzi mwaka 2010.

via blogu ya Mkwinda
 


Comments

mti mkavu
04/02/2012 00:29

Kumzomea mtu yeyete ni ushamba wa demokrasia, uhuni na ulimbukeni wa demokrasi. Tabia wanayo vijana wa CHADEMA ambao hapo kabla walikuwa hajui chocote kuhusu vyama vingi, sasa ndio wameelewa wajua vyama vingi ni fujo na matusi.

Reply
Bakari
04/02/2012 08:33

@mti mkavu, vipi tukisema kumzomea mtawala ni kuonesha kutorizishwa na utendaji wake katika nchi ambayo hata Bunge likiazimia kiongozi fulani astaafishwe kwa manufaa ya umma bado Rais wa nchi hafanyi hivyo!?

Serikali ya CCM ndio inayosababisha vijana wawazomee viongozi maana hakuna kinachoazimiwa na Bunge, Serikali ikakitekeleza. Tuliona issue ya Ngereja, ukafata ubabaishaji wa Luhanjo (akahachwa mpaka muda wa kustaafu ukafika), issue ya Jairo iko kimya utadhani alichofanya ni kizuri sana. Kumbuka issue ya Richmond, kama sio Lowasa kujiuzuru mpaka leo angekuwa PM na akina Karamagi na Msabaha wangekuwepo hadi leo.

Kwa haya madudu yote bado unaona kuzomewa ni ushamba... basi 2015 Watanzania wote watakuwa washamba.

Reply



Leave a Reply