Asasi ya kiraia Tweweza imezindua kampeni ya "Ni Sisi!" inayolenga kuwaamsha wananchi wa Tanzania kuhusu nafasi yao katika gurudumu la maendeleo. Kampeni hii inatumia
majukwaa mbalimbali ya vyombo vya habari kutoa hamasa kuwa dhana ya mabadiliko kwenye jamii yanachangiwa kwa kiasi kikubwa na mwananchi mmoja mmoja, kinyume na kusubiri na kutegemea serikali, wanasiasa, misaada, n.k.
Twaweza wanaamini kusimamia changamoto zinazotukabili na kushiriki kwa vitendo kwa wananchi ni vitu ambavo vinaweza kusukuma maendeleo endelevu.
Tazama video zifuatazo kuhusu sekta na maada mbalimbali kisha toa maoni yako. Itakuwa vizuri pia ukisambaza kwa Watanzania wengine.
1. Daladala/Matatu
2. Viwanja vya Michezo
3. Huduma za Afya
4. Daraja
5. Uchafuzi wa Mazingira
6. Uteketezaji wa Misitu