Hii ilikuwa ni siku maalumu ambayo Jumuiya hiyo ilimuaga rasmi katika wadhifa wake wa Ubalozi.
Mhe. Mwanaidi amesisitiza suala la upendo, ushirikiano na umoja baina ya Watanzania.
Amewahimiza Watanzania waishio ng’ambo kuiga jumuiya za wahamiaji wengine waliopo nchini Marekani ambao wana vituo (centers) vya kuwahudumia, akitolea mfano wa Turkish Center ambayo hutoa huduma ya shule, afya n.k. kwa wanajumuiya wake.
Amezungumzia suala analoulizwa mara kwa mara kuhusu uraia wa nchi mbili (dual citizenship) akitolea mfano wa ilivyotamkwa kisheria katika katiba ya Kenya, akashauri viongozi wa DMV kuandika barua na kuituma kwa njia ya barua pepe kwenda kwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba akisisitiza kuwa ofisi ya Ubalozi ipo tayari kutoa msaada katika ‘draft’ hiyo na ushauri pale itakapohitajika kuhusu suala hilo.
Mwishowe, amekuwa mkarimu kwa yeyote atakayefika Tanzania na akataka kuwasiliana naye binafsi, basi atumie namba yake ya simu ambayo itakuwa +255 78 426 8888.
wavuti.com inawashukuru Mubelwa Bandio na Abou Shatry wa Jamii Production kwa kutushirikisha video hii.

RSS Feed
