Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP), Dk. Eliezer Feleshi, amesema Baraza Kuu la Jumuiya na Taasisi za Kiislamu zinapaswa kwenda mahakamani kukata rufaa kama kuna uonezi wowote uliotolewa juu ya zuio la kutoa rufaa kwa katibu wa jumuiya hiyo, Shekh Ponda Isa Ponda, kuliko kuandamana.

Akizungumza na NIPASHE ofisini kwake jana, alisema chombo chenye mamlaka ya mwisho ya  kutoa haki ni mahakama na siyo kufanya maandamano. Alisema kama wanaona DPP amekwenda kinyume katika kutoa haki juu ya kupewa dhamana kwa katibu wao, wanapaswa kufuata sheria kwa kwenda mahakamani.

Alisema kwa mujibu wa katiba ya Jamuhuri ya Muungano Ibara ya 107(a)1 kinasema mamlaka yenye kauli ya mwisho ya utoaji haki katika Jamhuri ya Muungano ni Mahakama.

Alifafanua kuwa  kwa mujibu wa Ibara ya 59(b) Ibara ndogo ya nne kinasema Katika kutekeleza mamlaka yake, DPP atakuwa huru, hataingiliwa na mtu yeyote au na mamalaka yoyote.

Dk. Feleshi alisema Ibara ya 13(1) kinasema watu wote ni sawa mbele ya sheria, na wanayo haki, bila ya ubaguzi wowote, kulindwa na kupata haki sawa mbele ya sheria.
Mimi sijaona watu wanadai haki kwa maandamano, hii ofisi haina dini wa kabila, wala itikadi, wala sura, ofisi hii ni ya watu wote.
 


Comments


Your comment will be posted after it is approved.


Leave a Reply