wavuti
 
Hatimaye leo tarehe 10 Machi 2010 Dk. Hamisi Kingwangalla atangaza rasmi nia yake ya kuwania ubunge wa jimbo la Nzega kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Picture
Dk. Hamisi Kingwangalla
Dk. Hamisi A. Kigwangalla (MD, MPH, MBA) ni kijana msomi mwenye umri wa miaka 35, mwenye digrii tatu na aliyebobea katika taaluma ya afya ya jamii na utawala wa biashara. Dk. Kigwangalla ni kijana wa kitanzania anayeamini kwenye fikra mbadala na za kisasa lakini anaamini katika misingi iliyowekwa na wazee waasisi wa TANU na ASP. Alihitimu masomo ya digrii ya udaktari wa tiba ya binadamu (yaani Doctor of Medicine, MD) kutoka chuo kikuu cha Dar es salaam mnamo mwaka 2004. Pia ni muhitimu wa digrii mbili za uzamili; moja ambayo ni Masters in Public Health Sciences (major: Safety promotion) – kwa Kiswahili inatafsirika kama digrii ya uzamili katika sayansi ya afya ya jamii (amebobea kwenye kuhamasisha usalama), alihitimu mwaka 2007 kutoka chuo kikuu cha Karolinska Institutet, Stockholm, Sweden, na ya pili ni Masters in Business Administration (major: organization and leadership) – ambayo kwa Kiswahili inatafsirika kama digrii ya uzamili katika utawala wa biashara (amebobea kwenye mambo ya uongozi na miundo ya mashirika) aliyoipata kutoka Chuo Kikuu cha Blekinge (Blekinge Institute of Technology), pia kilichopo Sweden, mjini Ronneby.

Dk. Kigwangalla anaamini katika kutoa mchango wake juu ya maendeleo ya jamii kuliko kusubiri atafanyiwa nini na Taifa lake. (kama alivyowahi kusema raisi wa zamani wa marekani Bw. Abraham Lincoln).

Dk. Kigwangalla ni mtu anayefanya kazi zake kwa umakini, spidi na maarifa, na kuzingatia misingi ya maendeleo na uwajibikaji. Ni mwanapinduzi anayeamini mapinduzi ya Uchumi wa Tanzania yako karibu, na kwamba tutaendelea tu kama tutabadilisha fikra zetu (change of mindset). Anaiona Tanzania kama ni nchi yenye fursa nyingi na kwamba ni nchi iliyokaa vizuri na tayari tayari kuyapokea mapinduzi ya kiuchumi (Tanzania ni miongoni mwa emerging economies in Africa). Anaamini kuna haja ya kuwapa nafasi watu ambao wanayaona maisha kwa macho tofauti, badala ya kuangalia matatizo tu wanaangalia fursa ziko wapi ndani ya hayo matatizo. Bila kubadilisha mtazamo wetu hatutoweza kusonga mbele, itakuwa ni sawa na kujaribu kukimbiza jahazi nchi kavu!

Yeye anasema “maadui wa Tanzania wanajulikana na njia za kupambana nao zinajulikana – maadui hawa wapo toka nchi hii ianze, sasa kama maadui tunawajua na silaha za kuwamaliza tunazo, tunangoja nini sasa?....” Hapa anaongelea Ujinga, Maradhi na Umaskini.

Yeye anaona kuna ya haja ya viongozi mahiri na wenye nia thabiti ya kuwatumikia watu wajitokeze popote walipo na waje kuongeza nguvu kwa taifa letu ili tuweze kupambana na maadui hawa. Anasema, “tatizo kubwa ni kwamba watu wengi wanaogopa kuingia kwenye ‘mainstream politics’ kwa kuwa hawajiamini katika uwezo wao wa kukabili mikiki mikiki inayoendana na siasa, wengine wanafikiri siasa ina wenyewe, wengine wanasubiri wastaafu ndiyo waingie kwenye siasa (hivi utaweza kutawatumikia watu vizuri wakati ukiwa umechoka?). vijana wengi wasomi na wachapakazi wazuri kabisa wanasahau kwamba siasa na mfumo wa maisha yao ya kila siku na kwamba hadi majumbani mwao wanafanya siasa– wengine ni watu makini sana na wangeweza kuchangia mengi kwenye kuleta maendeleo ya taifa letu, ……tatizo kubwa ni kwamba watanzania ni wazuri sana wa kusema na kupanga lakini ni wavivu wa kutekeleza, hivyo tunahitaji viongozi watendaji kwenye kila sekta, popote walipo wafanye mabadiliko! Tuache kuongea na kupanga tu, sasa tuanze kuwa mabingwa wa utekelezaji!” “….pia viongozi wengi si wabunifu, wachovu wa kufikiri na hivyo hata utendaji na usimamizi wao wa sera nzuri zilizowekwa unakuwa mbovu”

Dk. Kigwangalla anasema kwa kuyaangalia yote haya na ametafakari kwa umakini na kujipima uwezo wake, ameonelea aanze kwa vitendo ili awe chachu ya mabadiliko kwa watu wa Nzega, ambako ndipo alipozaliwa. Anasema, “jamani Charity begins at home na ndo maana nimeamua kuwania ubunge wa Nzega ili nishiriki kikamilifu na kwa ukaribu zaidi pamoja na wana Nzega wenzangu katika kuzikabili changamoto za maendeleo katika jimbo la Nzega kwa spidi na kwa ubunifu wa hali ya juu…..maana mimi kila nikiiangalia Nzega sioni matatizo bali naona fursa tu za kuleta mabadiliko, nashindwa kuelewa kwa nini sasa watu wakose mahali pa kunyweshea mifugo yao wakati mungu ametujaalia mabonde na mito ya kumwaga kabisa? Siku moja nilipita kijiji cha Nata, ambacho kipo karibu kabisa na bonde la mto Manonga, nilishangaa na kusikitika sana kuwaona akinamama wakifuata maji mbali kabisa na miji yao, takriban kilomita tano au saba! Eti kijijini hakuna visima, kweli?” Nikafuatilia sana suala hili nikagundua kuwa tatizo haliishii hapo tu, wakazi wa vijiji vya sehemu moja huwa wanalazimika wakati wa kiangazi kupeleka mifugo yao kuwekeza kwenye vijiji vilivyo karibu na mto, kweli tumeshindwa hata kutega maji kwa ajili ya mifugo yetu?”

Japokuwa Nzega ina fursa nyingi, na ni mojawapo ya wilaya kongwe, kasi yake ya maendeleo haiendani na fursa zilizopo. Nzega ilikuwa ni wilaya ya mbele kimaendeleo tangu miaka ya 60, mzunguko wa hela ulikuwa mkubwa, miundo mbinu ilikuwa na hali nzuri zaidi ya sasa ukilinganisha na wilaya zingine, lakini kasi yake ya ukuaji hairidhishi na shughuli za uchumi na maendeleo zinazidi kuzorota siku hadi siku.

Dk. Kigwangalla anasema “kasi ya maendeleo ya Nzega hairidhishi na matatizo mengi ya msingi hayapatiwi ufumbuzi…kero zinazowakabili watu wa Nzega ni nyingi na zinahitaji mtu mwenye uwezo mkubwa wa kufikiri na kubuni miradi mbalimbali itakayoweza kuharakisha maendeleo ya Nzega. Wananchi wa Nzega wanahitaji kuwa na kiongozi mwenye kupenda maendeleo, mwenye fikra mbadala na mwenye uwezo wa kuanzisha msukumo mpya wa kasi ya maendeleo kulingana na kero zao na vipaumbele vya kisera na kimikakati vya kiwilaya na kitaifa.” “Kuna mambo mengi hayajakamilika na utekelezaji wake unalegalega – nyumba za walimu na baadhi ya vyumba vya madarasa kwenye mashule ya kata havijakamilika, waalimu hawatoshi kwenye shule zetu mpya; huduma duni za ugani kwa wakulima, hali ya miundo mbinu vijijini bado hairidhishi.”

Mke wangu siku moja aliniuliza swali, maana yeye huwa muoga sana na hapendi sana mikakati yangu ya kuingia kwenye siasa, “hivi kwa ni haswa unataka kugombea Ubunge? Si ufanye tu mambo yako?” Na mimi sikusita kumjibu kuwa: “Ninataka kugombea Ubunge kwa kuwa ni uwezo mkubwa wa kuwatumikia watu, nina wito na ni haki yangu ya msingi kikatiba”. Alivyo kin’gang’anizi akaendelea “kwa nini lazima wewe tu, si uwaache wengine wafanye?” Nikamwambia: “mimi naona kama mambo hayaendi inavyopaswa na ninajiona kama ninaweza kuyafanya kwa ubora zaidi, sasa kwa nini nisitoe mchango wangu kwa taifa? Nikamuuliza wewe ni daktari, umeshuhudia akinamama wangapi wakipoteza maisha kwa kukosa huduma, wengine wakizalia njiani bila msaada wowote wa huduma? Je haya mambo kama yakipata watu wenye nia ya kweli ya kubadili mambo hayatendeki?” akanyamaza. Kwisha kazi yake. “mimi nikiangalia mjane aliyeachwa na babu yangu mdogo pale Inagana, Magengati naona kama anahitaji msaada kidogo tu aweze kumudu kuendesha maisha yake. Ndugu zangu wanaolima vitunguu kule Milambo-Itobo hawahitaji vitu vikubwa sana, wanahitaji wapate mtu wa kuwatetea na kuwaongoza kidogo tu waweze kupata faida zaidi kwenye shughuli zao na waboreshe zaidi maisha yao. Ni watu kama hawa wanaonifanya nijisikie wito zaidi wa kwenda kushirikiana nao kuleta mabadiliko katika maisha yao na familia zao, naona kama wamewekwa pembezoni na hawana mtetezi!

Mzee wangu Mzee Masanilo ni mkulima stadi na mahiri sana, hahitaji vitu vikubwa wala vya kutisha, yeye anahitaji soko la uhakika tu la mazao yake ya pamba, alizeti na mpunga. Wadogo zangu, akina Fatu na Ibra wao wanahitaji uhakika wa kuendelea na masomo ya kidato cha tano na au vyuo vya kati (vya kutoa Diploma na Vyeti) vya kuwapa ujuzi na maarifa, wanahitaji madaraja ya kupandia chuo kikuu, wanahitaji hizi fursa ziwepo. Zote hizi ni kero, na tunazijua, je ni lini tutazifanyia kazi? Kwa nini tunashindwa? Ninajiona kama nina majibu ya maswali yote haya na ninadhani naweza kuyafanyia kazi ipasavyo.

Leo hii nimeamua kuiweka nia yangu hadharani kabisa kuwa kwa ridhaa yangu na matakwa yangu binafsi, nafsi yangu inanituma na hapa basi natangaza rasmi nia yangu ya kuvuta fomu kuwania ubunge wa jimbo la Nzega kupitia chama changu, Chama Cha Mapinduzi (CCM), pindi wakati utakapowadia. Naomba mungu aniongoze. Amina.

Dk. Hamisi Kigwangalla’s Contacts are:
0715636963
0754636963
0784636963

Email: hkigwangalla@gmail.com

Website: www.peercorpstrust.org

Blog: kigwangalla.blogspot.com

 
 
Picture
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na Makamu na Kaimu Rais wa Nigeria, Dk. Goodluck Jonathan kwenye hoteli ya Transcorp Hilton jijini Abuja anakohudhuria Mkutano wa Viongozi wakuu kuhusu maendeleo ya biashara na viwanda vya kilimo barani Afrika. Alimwakilisha Rais Jakaya Kikwete katika mkutano huo.
Picha kwa hisani ya Mroki Mroki
 
 
Picture
Several security websites are reporting a flaw in one telephone company that is transiting malware via HTC phone's USB port port when connected to computers.

A person recently bought an HTC Magic (Android) phone and when she connected it to her PC over USB, the antivirus (Panda) software went off.  The say that the phone had malicious autorun and other files identified as a "Mariposa" bot tied to a botnet run by a Spanish hacker. There was also Conficker and a Lineage password stealer.

Other smart phone users need to be aware of this threat in order to prevent their phones and computers from getting these malicious files that could severely affect their documents.

Click here to read and see screen capture of the  Vodafone HTC malware issue.

 
 
Learn how to create a long, complex, strong yet easy to remember password.

Katika posti iliyopita, tuliongelea juu ya namna ya kujiweka mbali na wezi wa mtandaoni kwa njia ya email lakini tuliacha kiporo cha kujifunza namna ya kutengeneza nywila ndefu, ngumu na madhubuti  na ambayo ni rahisi kuikumbuka. Leo tutajifunza kuhusu hilo.
  1. Tunga sentensi ambayo utaikumbuka. (Think of a sentence that you will remember).
    Mfano: "Nilisafiri kwa mara ya kwanza nikiwa na miaka kumi na mbili."
  2. Ibadili sentensi hii kuwa nywila. (Turn your sentence into a password).
    Tumia herufi ya kwanza ya kila neno katika sentensi yako uliyotunga hapo juu kutengeneza nywila. Mfano nskmyknnmknm
    Use the first letter of each word of your memorable sentence to create a string, in this case: "nskmyknnmknm".
  3. Ongeza ugumu katika nywila yako (Add complexity to your password or pass phrase).
    Changanya herufi kubwa na ndogo na namba na weka makosa ya lazima.
    Mfano: Tukitumia sentensi yetu ya awali, unaweza kubadili 'kumi na mbili' kuwa '12' kwa hivyo nywila yako sasa itakuwa, nskmyknnm12
    Mix uppercase and lowercase letters and numbers. Introduce intentional misspellings.
    For example, in the sentence above, you might substitute the number 12 for the word "kumi na mbili", so a password might be "nskmyknnm12".
  4. Ongeza alama maalum (Substitute some special characters).
    Tumia alama zinazofanana kwa ukaribu na herufi. Unganisha, ongeza au zitumie kubadili kabisa baadhi ya herufi. Hii itaongeza ugumu wa nywila yako.
    Mfano: n$kmyknnm12
    Use symbols that look like letters, combine words, or replace letters with numbers to make the password complex. Using these strategies, you might end up with the password "n$kmyknnm12" .
  5. Changanya herufi kubwa na ndogo (Combine capitals and small letters).
    Mfano: n$KmyKNNm12
Natumai hadi kufikia hapa utakuwa umeelewa namna ya kutengeneza nywila madhubuti. Ukitaka maelezo ya ziada, unaweza kusoma kupitia mojawapo ya tovuti hizi (bofya hapa).

Tunza nywila yako katika usiri. (Remember to treat your password as a secret).
Kwa vidokezo vilivyopita tafadhali peruzi kwenye 'Computer Or Email Tips & Tricks'.
 
 
Pata huduma murua na za uhakika kabisa za utalii nchini Tanzania kupitia  Real Adventure Safaris
Picture
Zephaniah S. Kambele (Zepha)
Real Adventure is a Fully Licensed reliable Tour Operator organizing safaris and tours to explore the nature of Tanzania. Real Adventure is run by a qualified team of professionals with over 20 years of combined experience in the travel industry. The vehicles and equipment used are of high quality. Our professional and experienced staff are always up to discuss and arrange proper itineraries.

Our focus is on QUALITY SERVICE and SAFETY! Combine this focus with the beautiful scenery and wildlife of Tanzania, Real Adventure is the ideal company to arrange your life time adventure. We specialize in wildlife safaris in all the National Parks and Game Reserves of Tanzania including the Serengeti National Park-endless plains, the Ngorongoro Crater-eighth natural wonder of the world, Lake Manyara- tree climbing lions, Tarangire, Mikumi, Ruaha and Arusha National Park; Selous Game Reserve and all other wildlife areas. A visit to Lake Eyasi for hunting with the Bushmen (Hadzabe is not to be undermined due t its unique)

Real Adventure also specializes in mountain climbing/trekking including Mount Kilimanjaro, Mount Meru and Oldonyo Lengai. Additionally, Real Adventure can combine these excursions with walking safaris, cultural tours, biking and Zanzibar beach holidays. We are a full service tour company: we will arrange your flights, book your accommodations, arrange for transfers, and much more. Real Adventure will guide you to and through the nature of Tanzania with quality service and your safety always in mind.

Picture
Apart from service other parts of the world, we highly encourage our fellow Tanzanians to allow us take them through the beautiful scenery of their own country. There are a lot of options ranging from one day trip to over 30 days trip. We have a long time experience and knowledge in customizing trips and this will surely be worth to you plan. Please let us know what you wish and we will discuss with you for a life memory trip.

You can plan a family trip during your holiday/leave from work, either a private trip or a joint trip with friend families to even make the costs down.

As you are looking for professional and experienced staff, high quality food and equipment, book with Real Adventure Co. Ltd.

Please feel free to visit our website www.realadventuresafaris.com for further information and whenever a need arises do not hesitate to contact us. Gideon, Eli, or Zephaniah (au “Zee” as just being baptized by Da Subi!) will be there to come back to you in time for a fruitful discussion/conversation.

Real Adventure Co. Ltd,
P.O. Box 16906,
Arusha.
Tanzania-East Africa.

E-mail: info@realadventuresafariscom
           realadventureltd@habari.co.tz

Website: www.realadventuresafaris.com

Tel (office):      +255 732 972 432
Emergency Number:  +255 787 316 205  (Egidius)
                               +255 782 062 949

Tourist Agency Licence (TALA) No. 00010520

Member of TATO
"Safari Experts in Tanzania - Locally Owned and Guided"
 
 
 
 
Picture
Ninite: The easiest way to add applications to your computer. Using ninite is as easy as:
  1. Go to ninite.com
  2. Pick the application(s) you need
  3. Start your customized installer
Ninite installs apps with default settings and says "no" to browser toolbars and other junk.
Ninite checks your PC's language and 64-bit support to install the latest, best version of each application.
Ninite runs on Windows XP/Vista/7 and works in the background 100% hands-free.
will not be installed in your PC

Ninite won't be installed in your PC, all it does is install the applications you choose.
Want to see how Ninite works? Here is a step-by-step walk through by How-To Geek (click here).

Website: ninite.com

 
 
Ninahisi tunastahili kabisa, sisi na viongozi wetu, kuandikiwa barua kama barua iliyoandikwa na gazeti moja la udaku ambalo ni maafuru sana pande za huko Ulaya, waliyoiandika barua hii ni baadhi ya Wajerumani wanaokusudia kufikisha ujumbe kwa wadeni wao ambao ni nchi ya Ugiriki kutokana na kushindwa kulipa deni wanalowiwa. Awali, baadhi ya wanasiasa nchini Ujerumani waliwaambia Wagiriki kuwa yawapasa wauze baadhi ya visiwa vyao ili waweze kulipia deni la Euro bilioni hamsini. Baadaye ndipo gazeti moja liliandika ujumbe wa barua kwa Waziri Mkuu wa Ugiriki bwana George George Papandreou unaosomeka hivi:
Picture
Dear prime minister,
If you're reading this, you've entered a country different from yours. You're in Germany.

Here, people work until they are 67 and there is no 14th-month salary for civil servants. Here, nobody needs to pay a €1,000 bribe to get a hospital bed in time.

Our petrol stations have cash registers, taxi drivers give receipts and farmers don't swindle EU subsidies with millions of non-existent olive trees.

Germany also has high debts but we can settle them. That's because we get up early and work all day.
We want to be friends with the Greeks. That's why since joining the euro, Germany has given your country €50bn.

 
 
Honda CRV. Model 2000. Automatic. 4 cylinder. Color: Metalic Golden. Imetembea mileage 47000 tu.
Bei ni maelewano kupitia +255784524148 na/au +255715524148
Bofya picha zifuatazo kuzikuza kwa muonekano mzuri zaidi
 
 
Picture
Anasikika aliyewahi kuwa mfungwa wa mojawapo ya magereza nchini Tanzania kwa kutuhumiwa kosa la ubakaji ambapo mahakama ilimhukumu miaka 30 ndani, hata na hiyo mfungwa huyo alitoka baada tu ya kutumikia kifungo hicho kwa miaka 9 kutokana na kukata rufaa na kubainika kuwa alifungwa kwa kosa ambalo halikuthibitika kutenda.

Tafadhali tembelea ukurasa wa Audios au bofya hapa upate kuikiliza kipindi hiki cha Njia Panda kilichorushwa hewani siku ya Jumapili, Machi 7, 2010 ndani ya redio Clouds FM.

Shukrani za pekee kabisa zimfikie Dk. Lelo Baliyima aliyerekodi na kututumia audio hii.