 Zitto Kabwe (Mb) Mwalimu Azaveli Lwaitama ni mwalimu na mlezi wangu nje ya darasa. Alipokuwa Katibu wa Umoja wa WanaTaaluma Chuo Kikuu cha Dar es Salaam mimi nilikuwa Mwanafunzi wa mwaka wa kwanza Idara ya Uchumi. Nilikuwa nashinda kwenye Ofisi ya UDASA tukijadiliana kuhusu Umajumui wa Afrika (Pan Africanism), Ujamaa na harakati za kulinda haki za watu. Ilikuwa ni nadra kwa Mwanafunzi wa Uchumi kuwa karibu na mwalimu wa Lugha na mnadharia mkubwa. Wanafunzi wa Uchumi tulikuwa tunajidai na kujivuna. Tulikuwa tunajiona bora sana maana darasa letu halikuwa linazidi watu 40 na kwa kweli wote hawamalizi. Darasa langu tulimaliza wanafunzi 25 tu kati ya 40 tulioanza. Mwalimu Lwaitama ni mpenzi mkubwa wa Muungano kama nilivyo mimi. Tumeapa kuulinda kwa namna yeyote ile. Yeye alikuwa mhafidhina sana akitaka muungano wa muundo huu aliouacha Mwalimu Nyerere. Mimi nataka kuulinda kwa kuufanyia marekebisho makubwa sana ya kimuundo. Hatukuwa tunakubaliana.
Wiki iliyopita Mwalimu Lwaitama kaandika kuhusu muundo wa Muungano katika makala zake za kila wiki katika Gazeti la kimombo la The Citizen. Amebadili msimamo. Ameona sasa muundo wa Muungano ulivyo sio endelevu. Ametoa mapendekezo niliyoyatoa siku za nyuma katika mazungumzo yetu ingawa yeye bado anayasema kwa shingo upande. Lwaitama sasa anataka Serikali mbili zilizonyumbuliwa. Anapendekeza Waziri Mkuu wa Muungano mwenye nguvu za za kitendaji. Nampongeza kwa kuboresha mawazo yake.
Hata hivyo bado Mwalimu wangu na Watanzania wengi wamejikita katika mjadala wa Serikali ngapi. Idadi ya Serikali inaonekana kama ndio dawa ya kero za Muungano. Ni kweli WaZanzibari wanataka uhuru zaidi na wengine hawataki kabisa Muungano. Unawalalia. Unawanyima uhuru wa kuamua baadhi ya mambo yao na japo halisemwi unawanyima wanasiasa wa Zanzibar mamlaka ya masuala mengine ambayo yangewafanya wajilimbikie madaraka.
Huku bara napo kuna watu, tena wanaongezeka kwa kasi kweli kweli, wakitaka Tanganyika yao. Tena wengi vijana. Demografia zetu zinaonyesha kwamba Watanganyika waliozaliwa Tanganyika ni takribani asilimia 12 tu ya Watanzania. Asilimia 70 ya Watanzania wamezaliwa wakati Muungano umeshasherehekea miaka 15 ya kuzaliwa kwake. Lakini wanataka Tanganyika yao. Wamechoshwa na kelele za WaZanzabari. Hawawataki WaZanzibari kujaa kwenye Bunge la Muungano wakati wapo kiduchu sana. Wanasiasa nao, japo hawasemi waziwazi wanataka wawe na mamlaka zaidi bila kulazimika kushauriana na wanasiasa wa Zanzibar. Linapokuja suala la wagombea Urais ndio kabisa wanakereka kutafuta mgombea mwenza kutoka Zanzibar. Wachambuzi wa historia za kisiasa siku wakiamua kufanya tafiti watachoka na roho zao watakapoona aina za wagombea wenza ambao wagombea Urais huteua, hasa kutoka sisi vyama vya upinzani.
Kiimsingi idadi ya wapinga muungano inazidi kuongezeka siku hata siku. Ukiwauliza kwa nini hawataki muungano wanasema aah, basi tu. Kama ni Mzanzibari atasema Tanganyika wanatutawala. Kama ni Mtanganyika atasema Wazanzibari wamezidi kelele, tunataka Tanganyika yetu. Sisi ‘Unionists’ nao hatuna majibu ya kuridhisha sana na kukonga nyoyo. Isipokuwa tu, Muungano huu ni wa iana yake Afrika na Duniani. Ni alama pekee ya kuonyesha Mwafrika kupinga mipaka ya kikoloni. Sasa hili haliwaingii kichwani ‘secessionists’ hatuna la kuwasaidia. Lakini ni lazima tuurekebishe Muungano huu. Ulivyo sasa utavunjika tu. Kuulinda muungano ni kuufanyia marekebisho makubwa. Mwalimu Lwaitama kaliona hilo. Pendekezo lake liboreshwe sasa. Sio rahisi sana.
Sasa tufanyeje? Serikali moja itaimeza Zanzibar. Serikali Tatu ni gharama kuendesha na Serikali mbili zimeimeza Tanganyika na watu wanataka Tanganyika yao na zinainyima uhuru Zanzibar na watu wanataka wawe huru zaidi. Mfumo wa Serikali ngapi na kadhalika ni moja ya mikakati ya wanasiasa katika kusaka vyeo. Sisemi sio halali kujadili lakini kiukweli mfumo gani wa Muungano hautaongeza fungu la dagaa kwa mwananchi wa Kagongo au sinia la ubwabwa kwa mwananchi wa Mkanyageni. Waingereza wana msemo ‘unataka kula keki yako na kubaki nayo’, basi tuwe na Serikali zote.
Nimeanza na Mwalimu Azaveli Lwaitama. Naboresha hoja yake kwa kurudia niliyowahi kuyasema huko nyuma kuhusu muundo wa Muungano. Tuwe na Dola Moja tu. Ndio, Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na wala sio Shirikisho la Tanzania (kwanza litatuondoa kwenye kiti chetu kule Umoja wa Mataifa maana kwa jina letu sisi tunakaa katikati ya Uingereza na Marekani. Katikakati ya mabwana wakubwa, labda ndio maana wanatupa misaada sana, unajuaje?). Tuwe na Rais mmoja tu mwenye mamlaka kamili ya Asasi za Dola – Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama, Uhamiaji, Sera za Fedha na jukumu la jumla la kusimamia ustawi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Achaguliwe na Watanzania wote wa pande zote mbili za Muungano kwa kupata zaidi ya nusu ya kura za pande zote za Muungano. Tuachane na mambo ya Mgombea Mwenza. Tumejaribu tumeona hana maana zaidi ya kutembea na mikasi tu.
Zanzibar iwe na Waziri Mkuu mtendaji kwa masuala yote ambayo sio ya Muungano. Tanganyika iwe na Waziri Mkuu mtendaji kwa masuala yote ambayo sio ya Muungano. Hawa watateuliwa na Rais wa Muungano kutoka chama chenye Wawakilishi wengi katika Baraza la Wawakilishi Tanganyika na Baraza la Wawakilishi Zanzibar. Wote watakuwa ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano kwa utaratibu kwamba iwapo Rais anatoka Zanzibar, basi Waziri Mkuu wa Tanganyika atakuwa Makamu wa Kwanza wa Rais na wa Zanzibar atakuwa Makamu wa Pili wa Rais. Kule kule kwenye misingi haswa ya Muungano. Hawa wataongoza Mabaraza yao ya Mawaziri na watakuwa na nguvu ya kuteua na kufukuza Mawaziri wanavyotaka. Hawatakuwa Wabunge katika Bunge la Muungano.
Bunge la Muungano litakuwa dogo lenye Wajumbe wasiozidi 101 pamoja na Rais wa Bunge la Muungano. Wabunge wa Muungano watatoka kwenye mikoa (au Majimbo kama sera ya Majimbo itakubalika). Kwa utaratibu wa sasa kila mkoa utachagua wabunge 2 mmoja mwanamke mmoja mwanaume kwenda Bunge la Muungano. Wajumbe wa Ziada watatokana na uwiano wa kura ambazo kila chama kimepata kwenye kura za Rais wa Muungano. Idadi hii yaweza kupunguzwa na hata kuwa na Wabunge 51 tu akiwemo Rais wa Bunge la Muungano ambapo kwa mikoa ya sasa kila mkoa utachagua Mbunge 1 na wengine watokane na uwiano. Rais wa masuala ya Muungano atakuwa Mkuu wa Shughuli za Serikali katika Bunge la Muungano na Rais kwa mwaka mara moja atahutubia Baraza la Taifa (Wabunge wa Bunge la Muungano na Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi kutoka kila upande wa Muungano). Wazungu wanaita hotuba hii ‘State of the Union’ na wengine huita ‘Queen’s Speech’.
Mkuu wa nchi mmoja, Dola moja ya Jamhuri ya Muungano. Serikali mbili na kila upande una Serikali yake yenye mamlaka kamili ya maisha ya watu wao ya kila siku. Haya, tatu pamoja na Serikali ndogo ya Muungano. Lakini tutakuwa tumepata kila kitu labda. Wenye kutaka Uhuru mpaka Zanzibar watapata. Wenye kutaka Tanganyika watapata na wenye kutaka Muungano kama Dola yenye nguvu watapata.
Kwani Waukraine hawa wanasema sema tu? Aa wapi, wanaishi "Walk the Talk!" Mjadala uliokuwa ukiendelea jana Alhamisi katika kikao cha Bunge huko nchini Ukraine kuhusu matumizi ya lugha ya Kirusi kwenye mahakama za nchi hiyo, hospitali na asasi nyingine za kijamii katika maeneo ambayo lugha kuu ya mawasiliano ni ile ya Kirusi, umezua malumbano ambayo yaliamsha hasira za baadhi ya Wabunge ambao waliposhindwa kujizuia walijikuta wakipindua meza na viti vyao kisha kukamatana mashati na kuchapana makofi na kuangushiana ngumi kiasi cha kutoana ngeu. "Fight once, and you'll always fight!" (kwa tafsiri yao wenyewe, siyo tunayoijua sisi)"Once a fighter, always a fighter" Hii si mara ya kwanza kwa Wabunge wa nchini humo kugeuza ukumbi wa Bunge kiwanja cha ndondi kwani mwaka 2010, tarehe 24 Aprili, Wabunge wa wakati huo walilabuana tena baada ya kushindwa kuafikiana tofauti zao kuhusiana na kuongeza muda kwa majeshi ya maji ya nchi ya Urusi kuwepo katika eneo linalomilikiwa na Ukraine ( bofya hapa kutizama video.)
Mbunge wa Rombo, Joseph Selasini amesema anayo kila sababu ya kuamini kuwa ajali iliyompata jana inachangiwa kwa kiasi kikubwa na uwepo wa bidhaa feki, (hapa akizungumzia matairi) bidhaa ambazo ni dhaifu kwa viwango vya bidhaa nchini zinazopimwa na kupewa kibali na shirika la viwango TBS.
Selasini amesisitiza kauli yake kwa kusema tairi la mbele la gari lililopasuka na kusababisha ajali aliyoipata jana huko Boma Ng'ombe, lilikuwa jipya kwa kuwa aliyabadili matairi yote siku chache kabla ya safari.
Vile vile ameliomba jeshi la Polisi nchini Tanzania kuendelea kutilia mkazo mafunzo kwa madereva na waendesha pikipiki kwakuwa wengi wao hawajui wala hawafuati sheria, kanuni na matumizi mazuri ya barabara na hivyo kuchangia kwa kiasi kikubwa kutokea ajali nyingi za vyombo vya usafiri na watumiaji wengine wa barabara.
Amesema ajali hii imemsababishia pengo kubwa ambalo hatakaa alisahau kamwe maishani mwake.
Bofya kifute cha pleya hapo kusikiliza taarifa hii kupitia kipindi cha Dira cha RSI - Uchambuzi wa matukio.
Taarifa ya Alois Komu aliyekuwa kwenye msafara
Naomba kuweka vizuri swala la ajali ya mbunge Selasini.
Nilikuwepo ktk msafara wa magari na tulikuwa pamoja Arusha kumzika padre Florid Mahoo, ambaye ni Shemejiye Mbunge. Katika gari lake alikuwa na Mamaye mzazi, Mama mkwe (yaani Mamaye marehemu Padre), Mke wake, Mwali wa Mama Mkwe wake, na Mama Mdogo wa marehemu Padre.
Alipata ajali kama inavyoelezwa na akina Mama hawa 4 (isipokuwa mke wake, walikufa), wawili palepale, mwali katika gari ya Polisi akipelekwa Boma hospitalini na Mamaye marehemu Padre njiani akipelekwa hospitalini KCMC.
Hakuwa anakwenda kumwangalia Babaye, japo kweli babaye yupo hospitali kwa muda tangu mwanzoni mwa mwezi huu.
Walio hospitalini kwa sasa ni Mbunge ambaye hali yake ni nzuri anaweza kuruhusiwa wakati wowote, ila mkewe aliumia shingo, mkono na sehemu ya kiuno na inaonekana yeye atakuwa hospitalini kwa muda. Tuwaombee wapokee misiba hii kwa utulivu wahusika wote, na walioumia wapone haraka. Marehemu wapumzike kwa amani amina, na Mungu awaangazie mwanga wa milele mbinguni.
- Alois Komu (akiwaandikia Wanamabadiliko)
Navi Pillay, the UN's Commissioner for Human Rights, wrapped up a five day visit to tense Zimbabwe this week, at the invitation of the coalition government. She has this startling advice for western nations that are punishing Zimbabwe over its poor human rights record: suspend international sanctions.
Pillay says the economic punishment has caused banks and investors to think twice about putting their money in Zimbabwe and that affects business. While the sanctions do target individuals, the overall effect hurts all poor Zimbabweans, who must also face political instability and crushing drought.
Here is her speech...
Speech by Ms Navi Pillay
United Nations High Commissioner for Human Rights at the University of Zimbabwe Harare, 24 May 2012
Distinguished Participants, Dear Students, Ladies and Gentlemen
I am very pleased to address you today at the University of Zimbabwe.
I would like to express my appreciation to the Government of Zimbabwe for inviting me to visit the country and for the welcome I have received.
This is the first visit by the UN High Commissioner for Human Rights to Zimbabwe. It follows Zimbabwe’s participation in the Universal Periodic Review (UPR), the mechanism which allows the Human Rights Council (HRC) in Geneva to review the human rights record of all UN Member States, during which Zimbabwe accepted 130 out of 177 recommendations made by other Member States. On the occasion of the adoption of Zimbabwe’s UPR report by the HRC Working Group on 12 October 2012, the Zimbabwe delegation noted that human rights should be viewed unselectively, objectively and in an un-politicized manner, and called for serious discussion, consideration and acceptance of social, economic and cultural rights. I welcome this indication from the Government of Zimbabwe of a willingness to engage seriously with the international community on human rights issues.
I fully agree that we need to advance all human rights comprehensively in the pursuit of full implementation of human rights. In my speech today, I will explore in some detail the protection and promotion of economic, social and cultural rights in the context of overall protection.
Indivisibility of rights
Duniani kweli tunatofautiana, labda wakikua wataacha. Pengine hata hawakukuzwa na dhana kama niliyokuzwa nayo mimi kuwa kuchezea chakula si sawa. Labda hawajui kuwa kuna watu wanakufa kwa njaa, ama pengine wanafahamu ila hawajali -- ni vigumu kung'amua. (picha: suxorz.com)
TAARIFA YA CHADEMA KURUGENZI ya Ulinzi na Usalama ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) inapenda kutoa taarifa kuwa matembezi ya wanachama wake kutoka maeneo mbalimbali ya Jiji la Dar es Salaam kuhudhuria mkutano mkubwa wa hadhara utakaofanyika Viwanja vya Jangwani, yako pale pale kama ilivyopangwa na kutolewa taarifa kwa Jeshi la Polisi.
Itakumbukwa kuwa mkutano huo wa hadhara utakaofanyika Mei 26, 2012 umeshakamilisha taratibu zote, ikiwemo kutoa taarifa kwa Jeshi la Polisi, ambalo tayari limesharidhia kushiriki kwa kutoa ulinzi kwa mkutano huo, siku hiyo ya Jumamosi.
Katika barua yetu ya Mei 23, 2012, kwenda kwa Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, tulisema kuwa kutokana na hamasa kubwa ambayo imejitokeza kwa wanachama wetu juu ya mkutano huo mkubwa wa hadhara, katika majimbo yote ya jiji na kutokana na hali halisi ya ugumu wa maisha unaowakabili wananchi wengi unaopelekea kutomudu gharama mbalimbali za maisha zikiwemo za usafiri (nauli za mabasi) wamejipanga kufanya matembezi ya amani, ya mshikamano, kuhudhuria mkutano wa Jangwani.
Katika mazungumzo na Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam leo, tumeona dhahiri kuwa jeshi letu linajenga hoja dhanifu zaidi na kufanya kazi kwa mtindo wa kupiga ramri badala ya kufanya kazi kisasa kwa kutumia hoja yakinifu zenye mantiki, katika kutimiza jukumu lao kubwa la ulinzi na usalama wa raia na mali zao.
Ni vigumu kwa mtu yeyote makini kuweza kukubaliana na hoja za Jeshi la Polisi kuwa hawataki wananchi watembee kwa amani kutoka maeneo mbalimbali kwenda eneo la mkutano eti tu kwa sababu kunaweza kuibuka vitendo vya ukabaji, uporaji katika matembezi hayo! Huku ni kufanya kazi kwa mtindo wa kupiga ramri!
Kumbukumbu zinaonesha kuwa hakuna maandamano yoyote ya CHADEMA yamewahi kuwa na vurugu au vitendo vyovyote vile vya uvunjifu wa amani isipokuwa tu pale ambapo Jeshi la Polisi liliingilia kati na kusababisha vurugu, likapiga watu, likatesa watu hata kusababisha vifo kwa visingizio na hoja zisizokuwa na msingi kama hizi wanazotoa sasa, huku wakitumia lile maneno yao maarufu 'taarifa za kiintelijensia'.
Pamoja na madai ya jeshi hilo kuwa hakuna askari wa kutosha kulinda matembezi hayo ya amani na mshikamano, kutokana na mantiki hiyo hapo juu, hatutashangaa wakipatikana askari wengi wa kuanzisha vurugu, kupiga watu, kutesa na hata kusababisha vifo, kama ambavyo imetokea katika maeneo mengine kwa kisingizio cha kuzuiamaandamano.
Imetokea hivyo Arusha, imetokea hivyo Songea (Ruvuma), imetokea hivyo Ikwiriri, Rufiji, ambako Jeshi la Polisi lenyewe limekiri wazi kabisa kuwa lilikuwa chanzo cha vurugu hata wananchi kupoteza maisha. Imetokea hivyo sehemu mbalimbali ambako polisi hudai hawana askari wa kutosha kuwalinda wananchi na mali zao, lakini wanapatikana askari wengi wakati wa kuvuruga na kupiga watu hata kusababisha vifo.
Tunawaomba ndugu zetu wa Jeshi la Polisi watoe ushirikiano kwa wananchi. Wasifanye kazi kwa ubaguzi wa aina yoyote ile katika makundi mbalimbali ndani ya jamii wala maelekezo ya kisiasa, hasa kutoka kwa chama tawala, CCM kama ambavyo imedhihirika mara kwa mara.
Tunapenda kusisitiza kuwa polisi wasifanye kazi kwa mtindo wa kupiga ramri na kujenga hoja dhanifu. Wanachama na wapenzi wa CHADEMA wamedhihirisha mara kadhaa, pasi na shaka yoyote kuwa wanaweza kufanya matembezi ya mshikamano bila kuathiri haki za watu wengine. Kwa amani na utulivu.
Tutaendelea kuthibitisha hivyo Mei 26, 2012, kuelekea Jangwani na mahali pengine popote ambapo tutatumia haki ya kikatiba kufanya matembezi ya mshikamano au kuandamana katika misingi ya kutoa elimu ya uraia kwa wananchi, kudai haki, mabadiliko ya kweli katika utawala na mfumo, kudai uwajibikaji wa serikali kwa watu au katika kupiga vita ufisadi na uonevu wa watawala dhidi ya wananchi.
Imetolewa Mei 24, 2012 Dar es Salaam na;
Wilfred Muganyizi Lwakatare Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama-CHADEMA TAARIFA YA POLISI JESHI la Polisi limepiga marufuku matembezi ya amani (maandamano) ambayo yameombwa kufanywa kesho na Chama Cha Demokrasi na Maendeleo (CHADEMA). Huku, jeshi hilo likibariki Mkutano wa chama hicho kufanyika kwenye viwanja vya Jangwani. Polisi limefikia hatua hiyo, baada ya kubaini kuwa hakuna sheria yoyote inayoruhusu chama cha siasa kufanya matembezi au maandamano isipokuwa mkutano. Mei 26 CHADEMA, kilituma maombi ya maandishi (barua) kwa jeshi hilo kuruhusu matembezi hayo ya amani, kutoka sehemu mbalimbali za jiji hadi viwanja vya Jangwani panapofanyika mkutano wa hadhara leo. Lakini jana Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam, Afande Suleiman Kova alisema, “Hakuna sheria yoyote ya Uchaguzi inayoeleza chama cha siasa kufanya matembezi, hivyo hatukubaliani na ombi lao lakini hili la mkutano ruksa kufanya hivyo” Kwa mujibu wa Kamanda Kova, CHADEMA iliwasilisha barua ya kuomba kibali cha kufanya mkutano, lakini kabla ya kujibiwa Mei 26 kiliwasilisha barua nyingine ili kupata kibali cha matembezi ya amani. “Walisema wanachama wao hawana nauli, kutoka kwenye maeneo ya jiji kwenda viwanja vya Jangwani, lakini mbona jana walifika Mahakama Kuu kwa magari na mabasi, kwa hili hatuwezi kukubali” alifafanua. Pia, polisi limesema mwanachama yoyote ambaye atapuuza amri hiyo, jeshi litamchukulia hatua za kisheria ikiwemo kukamatwa. Kamanda aliwaonywa Wanachama kutodanganyika na wakuu wao wa chama kwa kufanya matembezi hayo, kwani jeshi linamchukulia hatua za kisheria Mwananchi sio chama cha siasa.Kwa mujibu wa Kamanda huyo, jeshi la polisi halipendi kuona amri zake zikipindishwa, au kugombana na vyama vya siasa. Alienda mbali zaidi akisema, mji wa Dar es Salaam, unatakiwa kuwa na amani wakati wote, hivyo amri hiyo wana hakika itatekelezwa. Kwa upande mwingine Kova, alionya juu ya Mkutano huo wa leo, akisema uwe wa amani na utulivu. Alisema polisi wako tayari kutoa ulinzi wakati wote wa mkutano huo ili kuhakikisha kunakuwa na amani. -- taarifa via blogu ya Francis Dande vile vile kuna video (youtube)
Idadi ya watu waliopoteza maisha kwenye ajali ya gari la Mbunge wa Rombo, Joseph Selasini (CHADEMA), iliyotokea jana eneo la Boma Ng'ombe, wilayani Hai, mkoani Kilimanjaro jana jioni, imeongezeka na kufikia wanne. Jana watu watatu walifariki papo hapo ajalini, huku watatu wakiwahishwa katika Hospitali ya Rufaa ya KCMC ambapo mmoja wao, aliyekuwa mahututi amefariki leo. Waliopoteza maisha kwenye ajali hiyo ni pamoja na Mama Mzazi wa Mbunge huyo, Catherine Joseph Selasini (80), Agatha Jerome Mahoo (85) mkazi wa Rombo ambaye ni mkulima pamoja na wanawake wawili ambao hawajatambulika majina yao mmoja akikadiriwa kuwa na umri wa miaka 70 - 75 na mwingine 35 - 40. Majeruhi kwenye ajali hiyo ni pamoja na Mkewe Mbunge, Digna Kavishe (43)ambaye amepata majeraha sehemu za kichwa na hali yake siyo nzuri, pamoja na Mbunge mwenyewe, Joseph Selasini ambaye amepata majeraha kwenye bega pamoja na mkono wa kulia na hali yake inaelezwa kuwa inaendelea vizuri. Chanzo cha ajali hiyo kimetajwa kuwa ni mwendokasi pamoja na kupasuka kwa gurudumu la mbele baada ya gari hilo kuingiliwa na pikipiki mbele na kukosa mwelekeo. Miili ya Marehemu imehifadhiwa kwenye hospitali ya Rufaa ya KCMC kwa ajili ya taratibu za mazishi. Rodrick Mushi, Moshi/Tanzania Leo Gari lililopata ajali, la Mbunge wa Rombo (CHADEMA) Joseph Selasini
Naam, katika jamii yetu, jamii hii hii, hii yaimani zetu hizi za tawire, tayari tumekwishaanza kuhoji kilipokwenda kiatu cha Mheshimiwa na kama huko kilikokwenda kilikuwa/kiko salama... Hata kama kilianguka baada ya kulegea, wengine mm, hawaki.
Haya, na hawa wanafunzi kuwepo barabarani kwenye siasa wakati hukumu ya kesi inasomwa, muda wa vipindi vya kawaida wa skuli kuendelea, ndiyo waliahirisha masomo? walitoroka vipindi? au ushabiki wa siasa ukizidi, mara moja moja si mbaya?
Wanafunzi wa Shule ambao hawaweza kufahamika Shule wanayotoka wakishangilia ushindi wa Mnyika kwenye maandamano hayo wakiwa na picha ya Mbunge wa Jimbo la Ubungo John Mnyika (picha blogu ya Muhidini Sufiani) Mwanafunzi mwingine (picha: blogu ya Nyakasagani) picha: blogu ya michuzi-matukio.blogspot.com
|