Habari ndo hiyo kwa mujibu wa blogu mbalimbali, hapa ninanukuu kutoka blogu ya Basil Msongo - Maisha
Breaking NewsUnaweza kutizama picha za tukio hili ambapo Zombe na waliokuwa watuhumiwa wengine wanasindikizwa kwa vyombo vya kusalama kutoka eneo la mahakama kuelekea uraiani makwao. Picha zaidi zipo kwenye blogu ya John Bukuku - FullShangwe (bofya hapa) au bofya kwenye picha kuekelea huko.
WASHITAKIWA wote katika kesi maarufu iliyomuhusu aliyekuwa Kaimu Mkuu wa Polisi Dar es Salaam, Abdallah zombe na wenzake wanane wameachiwa huru.
Walishitakiwa kwa kosa la kuwaua watu wanne akiwemo dereva wa teksi na wafanyabiashara watatu wa madini wa Mahenge mkoani Morogoro.
Picha zaidi zinapatikana pia katika blogu ya Othman Michuzi - Mtaa kwa Mtaa
Washtakiwa wenzake na Zombe wakiwahi kupanda Land Rover ya Polisi (farasi mweupe) baada ya kuchoropoka katika kesi iliyowakabili takribani miaka mitatu.