Funny: The Priest and The Sheikh

Rafiki yangu Adam Lingson Mwamsiku anaye blogu kaitka UpoleSana.blogspot.com alisoma kichekesho cha "Funny: Huyu mtawa atakuwa amepinda!" kisha akaacha kichekesho chake pale Facebook, nikacheks kweli na muda mchache tena, rafiki yangu Stephen K akaniachia kichekesho kingine kilichonivunja mbavu, wacha niviweke hapa vikupe tabasamu. Kumbuka hivi ni vichekesho, hivyo usijeumia roho bure kwa jambo la utani:

From Adam
It reminded me of a story this guy told me; eti Padri na Sheikh wametoka zao nje ya nchi kwenye pipa. Misosi ilipogaiwa kwenye ndege padri akamshangaa sheikh anakataa soseji za pork; hee padri akamuuliza Sheikh vipi ndugu yangu mbona huchukui hii kitu? Sheikh akajibu; "Huwa sili kitimoto mie"; basi kwa mshangao akamwambia sheikh, "For sure u do not know what u r missing".

Walipotua DIA, na kutoka nje, kila mtu anachukua zake, basi viongozi wa dini hawa wakakumbatiana kuagana, Sheikh akamwambia Padri; "Mtumishi salimia familia yako!", hee kwa mara nyingine padri akashangaa! Ebo! hujui mimi sina familia; huwa hatuoi sisi!" Kusikia hivyo Sheikh mdomo wazi, Whaaaaat? ATI NINI???...HAMUOI?? HAKIKA, U DO NOT KNOW KNOW WHAT U pipo R MISSING!!"
From Steve
Watawa/masister watatu baada ya kutumikia parokia kwa muda mrefu walienda kwa paroko na kumuomba awaruhusu walao watende dhambi moja moja, baada ya kutafakari paroko akawaruhusu. Basi kila mmoja akatawanyika kwenda kujirusha kivyake. Waliporudi ilibidi kwenda kuungama kwa paroko. Sister wa kwanza akasema ametenda dhambi, kwa kutembea na mwanaume kwa mara ya kwanza maishani mwake; padre akamwambie nenda ukanywe maji ya baraka na dhambi yako itaondolewa. Wapili zamu yake ikafika akasema ametenda dhambi amempiga mpishi wa paroko, paroko akamwambia nenda ukanywe maji ya baraka na dhambi yako itaondolewa. Then akaja yule wa tatu, yeye akasema nimetenda dhambi kubwa; nimeyakojolea maji ya baraka...Padre mdomo wazi!!
everyoneneedsasmile8ui0gesillymonke.jpg funny smile monkeys image by summer_bumm