Mpaka lini hali hii jamani? WHY? Kwanini lakini?

Habari na picha nimezitoa kwenye blogu ya PwaniRaha.com, nimezitumia hapa na kwingineko kwa madhumuni ya kufikisha ujumbe huu ulio na sura ya uchungu na taabu ijapokuwa wanaoonekana kwenye picha wamevaa nyuso za furaha na pengine zenye matumaini. Ama kwa hakika Mwenyezi Mungu ni mwingi wa uvumilivu na ajua kuingia na kutoka kwa viumbe wake. Ole! Ole ni wao wanaojilimbikizia mali na kudhulumu haki ya mnyonge. Ole! Siku hiyo ya kiama, kwa hakika sitachelewa kusogeza kuni na vijinga vya moto ikiwa nitapewa kazi hiyo kwa kuwasogezea hao wanaojijua wanachokifanyia jamii hii ya WaTanzania. Naomba Mungu akupeni haki yenu stahili kwa kadiri ya nafasi zenu mlizopewa katika nchi hii na hayo mnayoyafanya. Mnajijua! Nami ninajijua vile vile katika nafasi yangu. Mungu na awape rehema wale wote wanaoteseka na kupata taabu kutokana na maongozi mabaya na yanayomnyima haki mnyonge, iko siku na siku yaja, wataelimika hawa, wataijua haki yao na wataidai haki hiyo kutoka mikononi mwa walioipokonya.
Ninaendelea kujifariji kwa maneno haya!

[1.JPG]
Mfanyabiashara ya Dagaa wa ziwa Nyasa katika soko kuu la Songea Ruvuma Editha Kiwila akipanga bidhaa yake ambao kisado kimoja huaza shilingi 2000 hadi 4000.(Picha na Albart Jackson.)

[2.JPG]
Akina mama ambao wanawauguza ndugu zao katika hosptali ya Wilaya ya Ludewe wakisonga Ugali nje ya wodi ya akina mama wanaosubiri kujifungua,kati ya akina mama 100,000.wajawaito 200 hupoteza maisha katika Wilaya hiyo kutokana na ukosekanaji wa miundombinu. (Picha na Albart Jackson)

[3.JPG]
Wanawake wajawazito toka katika vijiji 76 vinavyo zunguka Wilaya ya Ludewa wakiwa wamelala na wengine wakila chakula huku wakiwa wamesubilia siku zao za kujifungua katika hospitali ya Wilaya ya Ludewa Mkoa wa Iringa kati ya akina mama 100,000 wajawazito 200 hufariki kutokana na ukosefu wa huduma.

[4.JPG]

Inasikitisha: Baadhi ya akina mama wajawazito wakiwa nje ya wodi ya wazazi katika hospitali ya Wilaya ya Ludewa ambapo jengo hilo lina vitanda 6 na kila kitanda hutumiwa na akina mama wajawazito wawili. Wengine hulazimika kulala chini.