Mshindi na Washiriki wa Faidika na BBC 2009

 
Jane Mweni (Kenya)

Mshindi wa donge nono la fedha zenye thamani ya dola za Marekani 5000 wa shindano la Faidika na BBC 2009 ni dada Jane Mweni (umri miaka 21) kutoka Kenya aliyetoa mchanganuo wa mradi wa Kuzoa Takataka katika Jiji la kitalii la Mombasa ambamo yeye mwenyewe ni mkazi wake.

Orodha na nafasi za ushindi zilikwenda kama ifuatavyo:
  1. Jane Mweni (Kenya) - mradi wa Kuzoa Takataka katika Jiji la kitalii la Mombasa
  2. Mbaraka Juma (Tanzania) - biashara ya kufuga vyura na panya vitakavyotumika na shule za msingi na sekondari pamoja na taasisi za elimu ya juu kufanya utafiti wa kisayansi.
  3. Nyota Anjelique (Congo DRC) - biashara ya mafuta ya mawese.
Washindani wengine walikuwa: Chiza Bonye (Burundi), Hakizimana Aladin (Rwanda) na Gakuo Roy (Uganda).

Mbaraka Juma (Tanzania)
 
Nyota Anjelique (Congo DRC)
Chiza Bonye (Burundi)
Hakizimana Aladin (Rwanda)

 
Gakuo Roy (Uganda)


Blogu hii inatoa pongezi kwa vijana wote wanaojitahidi kushiriki katika mashindano haya na shughuli endelevu zinazowapa mbinu za kukabiliana na hali za maisha ya sasa na pengine baadaye.

Habari na picha kwa mujibu wa  BBC Swahili