Ni unyama usiopimika huu!

Nimesikiliza kwa uchungu mkubwa na masikitiko kisa cha mtoto aliyebakwa na wanaume wanne jijini Dar Es Salaam nchini Tanzania. Kisa hiki kilirushwa hewani na Gea Habib pamoja na Dina Marios katika kipindi cha Hekaheka cha CloudsFM radio tarehe 14 mwezi Agosti mwaka 2009 na kuwekwa mtandaoni katika tovuti ya DulloNet.com.
Nimesikitishwa hasa baada ya kufahamu kuwa mtoto aliyefanyiwa kitendo hiki cha kinyama na cha kuvunja utu wa binadamu kuwa hakujihusisha kwa hiari yake na biashara ya ukahaba. Kina na maelezo zaidi kuhusiana na habari hii sinayo zaidi ya nilichokisikia, ni matumaini yangu kwa kukiweka hewani kitasababisha hatua muafaka zichukuliwe dhidi ya unyama huu.
Nimejaribu kuwaza ni kwa nini watu wafikie hatua ya kufanya unyama wa aina hii, sijapata jawabu. Mambo kama haya yanachangia kabisa kuondoa imani katika ubinadamu na duniani kuendelea kuwa mahali pa hatari sana pa kuishi.