Picha: Ajali katika bweni la Idodi, Iringa

Picha zote na maelezo yanayoambatana nazo ni mali ya Francis Godwin zimepigwa naye na kupatikana kwenye blogu yake ya Ni Matukio Daima

Naibu waziri wa elimu na mafunzo ya ufundi Mwamtumu Mahiza na viongozi mbali mbali wa Serikali na chama mkoa wa Iringa na Taifa wakiangalia miili ya wanafunzi 12 wa Shule ya Sekondari Idodi walioteketea kwa moto usiku wa kuamkia leo Jumapili

Miili 12 ya wanafunzi wa Shule ya Sekondari Idodi iliyoteketea kwa moto usiku wa kuamkia leo

Naibu waziri wa elimu na mafunzo ya ufundi Bibi Mwamutum Mahiza akilia kwa uchungu mara baada ya kushuhudia miili ya wanafunzi waliokufa kwa moto uliotokana na mshuamaa katika bweni la wasichana Shule ya Sekondari Idodi wilaya ya Iringa usiku wa kuamkia leo, jumla ya wanafunzi 12 wameteketea kwa moto na kubaki majivu huku 22 wakijeruhiwa vibaya.

Mabaki ya miili ya wanafunzi wa kike 12 walioteketea kwa moto katika Shule ya Sekondari Idodi Wilaya ya Iringa Vijijini usiku wa kuamkia Jumapili.

Napenda kukuomba radhi mpendwa msomaji kwa picha hii ya kutisha japo hii nimechagua iliyonafuu kidogo.