Serikali ya Muungano Tanzania yakata rufaa dhidi ya Zombe na Wenzie

Mahakama ya rufaa nchini Tanzania imethibitisha kupokea rufaa iliyowasilishwa na Serikali dhidi ya Zombe na wenzie kwa kupinga uamuzi wa Mahakama Kuu wa kuwaachia huru washtakiwa tisa wa kesi wa mauaji ya wafanyabiashara watatu na dereva teski mmoja mnamo mwezi Januari mwaka 2006.


Msajili wa Mahakama ya rufani nchini bw. Francis Mutungi ameyasema hayo jijini Dar Es Salaam kuwa rufani hiyo namba 254 ya mwaka 2009 imeshapokelewa na kinachoendelea hivi sasa ni hatua za kuchukuliwa kwa kumbukumbu za kesi husika kutoka mahakama kuu ya Tanzania iliyoanza mwezi Septemba mwaka 2006.


Mutungi amesema katika rufani hiyo Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania imekata rufaa dhidi ya Zombe na wenzake walioachiwa huru mwanzoni mwa juma hili.


Mapema katika notisi yake ya Serikali aliieleza kuwa ushahidi uliotolewa katika kesi hiyo dhidi ya Abdallah Zombe na wenzake wanane ulikuwa unatosheleza kwa watu hao kutiwa hatiani.