TTaarifa sahihi: Hakuna harambee/mchango kwa Peter Owino

NDUGU JAMAA NA MARAFIKI,

FAMILIA YA OWINO INATANGULIZA SHUKRANI TELE KWENU NYOTE MLIOTOA HUDUMA YA AWALI/HARAKA KWA KAKA YETU PETER MARA ALIPOFIKISHWA HOSPITALI YA BUGANDO KWA MATIBABU MARA BAADA YA KUVAMIWA NA MAJAMBAZI AKIWA SAFARINI KWENDA SHIRATI KUPITIA BARABARA KUU YA KATI.

KHERI PIA KWA MADAKTARI WOTE WA BUGANDO KWA TIBA NZURI NA MAKINI.

SHUKRANI PIA KWA MARAFIKI NA WATANZANIA WOTE WALIOPATA FURSA KUMJULIA KHALI NA KUTUMA SALAAM ZA TIBA NJEMA NA MAOMBI YA UNAFUU WA HARAKA. MUNGU AWABARIKI.

AIDHA TUNAWASHUKURU MLIOHUZUNIKA ZAIDI NA KUTAKA KUANDAA MICHANGO YA ZIADA ILI KUSAIDIA KTK HUDUMA YA TIBA KWA PETER. NAOMBA NIWAHAKIKISHIE KUWA TUNATHAMINI ARI YA UPENDO HUO LAKINI FAMILIA IMEWEZA NA INAENDELEA KUMUDU HUDUMA ZOTE ZA TIBA VIZURI KWA SASA. PETER AMETOKA HOSPITALI NA ANAPONA HARAKA NYUMBANI.

FAMILIA HAIJAANDAA UTARATIBU WOWOTE WA MICHANGO NA TAFADHALI MASHAURI KAMA HAYA LAZIMA YAWE NA IDHINI YA FAMILIA.

KWA UPENDO NAWASHUKURU NYOTE, MUNGU AWABARIKI.

Maina Ang'iela Owino

k.n.y FAMILA YA OWINO