Ubunifu wa Bernard Kiwia wa baiskeli randaBernard Kiwia ni mshiriki kutoka Arusha, Tanzania katika maonesho ya 'Maker Faire Africa' ambayo ni sehemu ya kundi la IDDS ambalo linajihusisha na utengenezaji wa nyenzo za aina mbalimbali. Maonesho hayo yanayofanyika nchini Ghana na mshiriki wetu kutoka Tanzania aliweza kuonesha kwa vitendo mashine ya kusukuma kwa mkono ili kuranda mbao. Baiskeli aliyobuni imetokana na baiskeli inayotumiwa na walemavu wa miguu. Video hii hapa inaonesha kwa ufupi kabisa jinsi kifaa hicho kinavyotakiwa kufanya kazi. Ni matumaini yangu kuwa wabunifu na wajasiri-amali wa aina hii watapata ufadhili wa kuwawezesha kufanikisha malengo yao, jambo ambalo litawasaidia watu wengine kama vile walemavu wa miguu kuweza kufaidika na ubunifu wao na hatimaye kuongeza wigo wa ajira huku utegemezi ukipungua.

Picha zimepigwa na WhiteAfrican. Unaweza kuona picha nyingine zaidi kwa kubofya hapa.