Video: Ujumbe wa Koffi Annan kwa lugha ya KiSwahili

Ujumbe kutoka kwa aliyekuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Kofi Annan (2005) unaohimiza uhifadhi wa sanaa za miamba za Afrika. Kwa usemi wake, sanaa hizi ni miongoni mwa kumbukumbu za kale zinazoonyesha uwezo wa mwanadamu kufikiria. Ni sanaa inayoonyesha chimbuko la ubunifu wa binadamu. Ni utajiri ambao hauwezi kurudishwa pindi ukipotea. Lakini sanaa hii ya Kiafrika, haionyeshi tu Afrika ya kale, bali pia, Afrika ya leo na ya kesho. Wanasayansi, wanahistoria, wasanii na wanafunzi lazima wajifunze umuhimu wake katika miongo na karne zijazo. Zanaa za miamba za Afrika ni urithi wa pamoja wa Waafrika na binadamu wote, zawadi ya utamaduni kutoka kwa mababu zetu ambayo inaweza kuwaleta pamoja watu wenye asili mbalimbali wakiwa na lengo la kutumia pamoja na kuihifadhi isipotee.