Ajira KKKT - Dayosisi ya Mashariki na Pwani, Tanzania


EVANGELICAL LUTHERAN CHURCH IN TANZANIA
(Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania)

DAYOSISI YA MASHARIKI NA PWANI
(Eastern and Coastal Diocese)

Tel:.022-2125505, 2113246, Fax: 2125505

Office of: Social Service Dept.
Our Ref:  DMP/NKM: HJ/2009/3
Your Re: …………………………………..P.O. Box 837
Dar es Salaam
Tanzania 
                                                                                                                                                     25/09/2009

MKUU WA JIMBO/MCHUNGAJI/WAPENDWA KATIKA KRISTO,

Bwana Yesu Kristo Asifiwe,

YAH: TANGAZO LA NAFASI ZA AJIRA KATIKA DAYOSISI YETU.

Ninayo furaha kuwatangazia kuwa KKKT: DMP inazo nafasi nne (4) za ajira katika Idara yake ya Huduma za Jamii kama ifuatavyo:-

NAFASI            1.
           AFISA UTABIBU CLINICAL OFFICER.
WAJIBU  WAKE
Atawajibika kwa Mkurugenzi wa Afya wa Dayosisi.
KAZI/MAJUKUMU YAKE
Atasimamia na kuendeleza zahanati.
Atatoa huduma ya kwanza kwa maradhi ya kinamama na watoto.
Atashughulikia na kuratibu hatua za kinga na tiba
Atachunguza na kushughulikia maradhi ya kawaida
Atahakikisha huduma bora za utabibu zinatolewa vyema katika zahanati.
Ataboresha mahusiano na wadau wa afya hasa serikali na taasisi zingine
Atasimamia na kuratibu utoaji wa huduma za VVU/UKIMWI.
Atatekeleza na kusimamia program za afya ya msingi.
Atahakikisha miongozo na taratibu za kiafya za wizara zinafuatwa kikamilifu
Na atashughuli zingine zitakazopangwa na Mkurugenzi wa Afya

SIFA ZINAZOTAKIWA
Awe na Diploma au zaidi katika masomo ya utabibu toka katika chuo kinachotambuliwa na serikali.


UZOEFU
Miaka mitatu au zaidi katika kazi hiyo
NGAZI YA MSHAHARA
Maelewano kwa kuzingatia taratibu na viwango vya Dayosisi.

NAFASI      2.
MRATIBU WA KITUO CHA UDIAKONIA.


UWAJIBIKAJI
Atawajibika kwa Naibu Katibu Mkuu pamoja na kwa Afisa Mkuu wa Huduma za Jamii wa Dayosisi.

KAZI /MAJUKUMU YAKE
Atakuwa ndiye mkuu wa kituo hivyo atahusika na shughuli zote za kiutawala za kituo ikiwemo shule na vitengo vingine.
Atakuwa mwenyekiti wa menejimenti ya kituo.
Atakuwa mwenyekiti wa kikao cha watumishi wote kituoni.
Atakuwa Katibu wa Bodi ya Udiakonia
Atawajibika kushirikiana na uongozi wa Idara kutafuta wafadhili.
Atahusika kusimamia miongozo, será na maelekezo ya Dayosisi kituoni kwake.
Atawajibika kupanga mipango na mikakati ya kimaendeleo ya kituo katika kuwasaidia watoto wenye ulemavu wa akili.
Atahusika katika kuratibu ziara za kimafunzo, za wanaojitolea, n aza wageni wote watakaotembelea kituoni.
Kwa kushirikiana na walimu kituoni hapo ataratibu ziara zote za kimafunzo za watoto pamoja na walimu na wafanyakazi wengine.
Atakuwa kiunganishi katika ya wazazi wa watoto, viongozi wa serikali za mtaa katika eneo lao na Dayosisi katika kuwahudumia watoto wenye ulemavu wa akili.
Atashirikiana na Chaplain wa kituo katika utoaji wa huduma za kiroho na pia kuandaa ziara za kutembelea sharika na mitaa.
Atakuwa mjumbe katika kamati ya shule.
SIFA ZINAZOTAKIWA
Awe mwenye elimu ya Diploma ya juu au zaidi katika taaluma ya Ustawi wa jamii/sosholojia/maendeleo ya jamii/Elimu ya Ulemavu wa akili au viungo (OT) toka katika chuo kinachotambuliwa na serikali. 
Awe na ujuzi wa kutumia kompyuta ni muhimu.

UZOEFU
Awe mwenye uzoefu mkubwa wa uongozi wa miaka mitatu au zaidi.
Awe mwenye uzoefu na masuala ya watoto wenye ulemavu atapewa kipaumbele.

NGAZI YA MSHAHARA
Maelewano kwa kuzingatia taratibu na viwango vya Dayosisi.NAFASI        3.
MRATIBU WA HUDUMA ZA JAMII JIMBONI.UWAJIBIKAJI
Atawajibika kwa Afisa Mkuu wa Huduma za jamii wa Dayosisi.
Atawajibika kwa Afisa mipango, fedha na Utawala wa Jimbo.


KAZI/MAJUKUMU  YAKE
Atapanga, kuratibu na kutekeleza mipango ya ustawi wa jamii jimboni
Atabuni na kutekeleza miradi ya ustawi wa jamii na maendeleo.
Atasimamia na kuratibu utoaji wa misaada na huduma za kiutu kwa jamii hasa watu wenye ulemavu, yatima, wajane, waliopatwa na majanga mbalimbali n.k.
Atashirikiana na Mkuu wa jimbo na Afisa wa jimbo kubuni na kuanzisha fursa za kuwezesha na kuvijengea uwezo vikundi maalum kama wanawake, watoto, vijana, wazee katika miradi yao ya kuzalisha mali na kupambana na umaskini, ujinga  na maradhi.
Atabuni miradi ya kupambana na UKIMWI, Umaskini na Ujinga.
Atahakikisha maazimio na será za DMP za utoaji huduma bora kwa jamii zinafuatwa na kutekelezwa ipasavyo.
Atafanya kazi nyingine kadri atakavyopangiwa na wakuu wake wa kazi katika jimbo na Dayosisi.
SIFA ZINAZOTAKIWA
Awe mwenye Diploma au zaidi ya Ustawi wa jamii, Sosholojia, maendeleo ya jamii au inayofanana na hizo toka katika chuo kinachotambuliwa na serikali.  .
Awe na ujuzi wa Kutumia Kompyuta ni muhimu.


UZOEFU
AWE UZOEFU WA KAZI USIOPUNGUA MIAKA MITATU.


KIWANGO CHA MSHAHARA
Maelewano kwa kuzingatia taratibu na viwango vya Dayosisi.


NAFASI
 1. “FIELD WORKER” -Mradi wa kutembelea watoto majumbani (HVP)
KAZI NA WAJIBU  WAKE
Atahudumia watoto wenye Ulemavu wa akili.
Atatembelea watoto wenye ulemavu wa akili majumbani
Kushauriana na wazazi wenye watoto na kupanga mikakati na mbinu za kuwasaidia na kuwatunza watoto wenye ulemavu wa akili.
Atashirikiana na Mratibu na Meneja wa mradi katika kuwatafuta na kuwafikia watoto wengi zaidi majumbani.
Atashirikiana na maafisa ustawi wa jamii wa serikali, watendaji kata na viongozi wa serikali za mitaa katika kutekeleza vyema mradi huu.


SIFA ZINAZOTAKIWA
Awe mwenye Cheti cha Ustawi wa jamii/Sosholojia/maendeleo ya jami, Elimu ya Ulemavu wa akili/viungo (OT) au zinazofanana na hizo toka katika chuo kinachotambuliwa na serikali.
Awe mwenye uzoefu wa kulea na kutunza watoto wenye ulemavu.
Awe mwenye uwezo wa kuendesha pikipiki.
Wanaume watapewa kipaumbele.

UZOEFU
Awe wenye uzoefu wa si chini ya mwaka mmoja katika utoaji wa huduma majumbani.
Awe mwenye uzoefu wa kuhudumia watoto wenye ulemavu atapewa kipaumbele
NGAZI YA MSHAHARA
Maelewano kwa kuzingatia taratibu na viwango vya Dayosisi.

Hivyo KKKT: DMP inakaribisha barua za maombi ya ajira kwa watu wote wenye sifa zilizoonyeshwa hapo juu.


MAHITAJI MUHIMU KWA WAOMBAJI WOTE:
 • Barua ya maombi yako yaambatane na wasifu wako (CV) wenye wadhamini watatu na mawasiliano yao, picha ndogo (Passport size), Nakala ya vyeti halisi vya elimu na kuzaliwa,Nakala za mafunzo ya ziada na kompyuta, Barua ya utambulisho toka kwa mchungaji wa usharika wako
 • Uwezo na uzoefu wa kuongea, kuandika na kusoma lugha ya Kiswahili na kiingereza ni muhimu
 • Umri wa waombaji usizidi miaka 45.
 • Barua zote za maombi ziwe na nambari za simu.
 • Waombaji wenye sifa zaidi zinazotakiwa watapigiwa simu kwa ajili ya usaili utakaofanyika kabla ya tarehe 18/10/2009; HIVYO USISUMBUKE KUPIGA SIMU!
 • Waombaji Watanzania watapewa kipaumbele zaidi.
 • MWISHO WA KUPOKEA MAOMBI NI IJUMAA TAREHE 09/10/2009; SAA 8:30 mchana; MAOMBI YOTE YATUMWE KWA ANWANI IFUATAYO:-
KATIBU MKUU,
KANISA LA KIINJILI LA KILUTHERI TANZANIA,
DAYOSISI YA MASHARIKI NA PWANI,
LUTHER HOUSE, Ghorofa ya kwanza,
SOKOINE DRIVE,
S.L.P 837,
DAR ES SALAAM. 

Ni matumaini yangu kuwa tangazo hili litawafikia walengwa kupitia ofisi yako ili tuweze kupata watumishi bora kwa kazi ya Bwana wetu Yesu Kristo.

Wenu katika utumishi mwema wa Bwana wetu Yesu kristo,

ROBERT CHARLES
NAIBU KATIBU MKUU: HUDUMA ZA JAMII

NAKALA:-
 • BABA ASKOFU
 • MSAIDIZI WA ASKOFU
 • KATIBU MKUU
 • NAIBU KATIBU MKUU: UTAWALA NA UTUMISHI
 • NAIBU KATIBU MKUU: MIPANGO NA FEDHA
 • MHASIBU MKUU
1