Ambwene Yesaya (AY) kuzuru Malaysia | Ahitaji pia kura yako


WaTanzania wote waliopo Malaysia na pande za Asia kaeni tayari kumpokea msanii maafuru wa muziki wa kizazi kipya Ambwene Yesaya aka AY ambaye anatarajiwa kufanya onesho la muziki nchini Malaysia.
Tarehe:Alhamisi, 24 Septemba 2009
Jiji: Kuala Lumpur
Ukumbi:Titanium

Show hii itapambwa pia na wasanii maafuru kutoka Afrika wakiwemo upcoming artists kama IJL wa kundi la F.B.G tokea pande za Arusha  ambao wameshafanya kazi na wanamuziki maarufu nchini kama CPWAA na Nako 2 Nako (bofya hapa usikilize kibao kimojawapo).

Pia unakumbushwa kumpigia kura AY ili ashinde katika kinyang'anyiro cha MTVbase Award kupitia mama.mtvbase.com (bofya hapa)