Big up Kibasila pupils and students. Action speaks louder than words!

Wakati mwingine inabidi 'to take matters at your own hands' hasa pale uhai unapokuwa hatarini. Huwezi kuzembea wakati uhai wako unapohatarishwa. Uhai unao mara moja, baada ya hapo hakuna mwenye uhakika asilimia mia moja ikiwa unapoondoka duniani unarudi tena ama ulikokwenda ndo hurudi hadi siku ya kupulizwa parapanda. Ikiwa uhai utaondoka kizembe kwa ajali zinazozuilika, basi bora kuutetea na kuunusuru ama bora upotelee mbali katika harakati za kutaka kuuokoa!

Pichani ni wanafunzi wa sekondari ya Kibasila Dar es salaam wakiwa wamezuia magari kupita leo asubuhi katika makutano ya barabara za Chang'ombe na Mandela,kufuatia wanafunzi kugongwa mara kwa mara eneo hilo

WANAFUNZI wa Shule ya Sekondari Kibasila na Shule ya Msingi Kibasila leo walikua na mgomo kutokana na eneo hilo kuwa na ajali za mara kwa mara kusababisha vifo kwa wanafunzi wa shule hizo. Tukio hilo lililotokea leo asubuhi ambapo wanafunzi wawili wa shule ya msingi kibasila waligongwa na mwananchi mmoja ambaye alikua akiwavusha barabara kugongwa na hali yake sio nzuri na yuko hospitali ya temeke kwa matibabu zaidi.

Kwamujibu wa mashuuda wa tukio hilo walisema kuwa wanafunzi waliogongwa ni Consolatha Kilasa, Wiliston Sango wote wa darasa la 5  waliokuwa wakitoka nyumbani kuelekea shuleni ata hivyo jina la msamaria mwema halikupatikana. Akiongea na gazeti hili mmoja wa walimu alisema kuwa mwanafunzi mmoja aliyejulikana kwa jina Wiliston Sango yupo hospitali ya mifupa (MOI) kwa matibabu  zaidi kutokana na kujeruhiwa vibaya.

Pia katika tukio hilo wanafunzi waliweza kuzuia baadhi ya magari yasipite katika eneo hilo likiwamo gari la  jeshi lenye namba za usajili 2813 JW97 Defender na gari la polisi PT-0176.

Makamu  mkuu wa shule ya kibasila mwalimu Catherine Urio alito wito na kuomba wakala wa barabara kuweka matuta,taa,alama za pundamilia na askari wa kuongozea magari kwani kutokuwepo kwa vitu hivyo kunasababisha ajali nyingi na watu upoteza maisha kwa wingi.

Hatahivyo Wanafunzi walisema kuwa hawataki kusikia siasa zinatendeka wanachotaka wao matuta yawekwe na taa pia trafiki awepo katika barabara hiyo ya changombe.

Wakati huo huo mwenyekiti wa serikali za mitaa  Sophia Kinega alisema ni halali kwa wanafunzi kufanya mgomo huo kwani ajali nyingi zinatokea na kuua wanafunzi mara kwa mara kwani  wanafunzi hao wanaona uchungu kuona wenzao wakipoteza maisha.

Mkuu wa Wilaya  ya Temeke Jordan Lugimbano aliwataka wanafunzi aongee nao ila wanafunzi hao walionekana wakimzomea,baada ya  muda wanafunzi walikubali na kwenda kuongea nae iliwaweze kutafuta ufumbuzi wa tatizo hilo. - Darleo.co.tz