Breaking News: Mabomu yalipuka tena Mbagala

Kwa mujibu wa blogu ya Basil Msongo, http://simulizi.blogspot.com

MABOMU yamelipuka Mbagala muda mfupi uliopita.
Kuna taarifa zinazodai kuwa watu wawili wamekufa, wengine kadhaa wamejeruhiwa.
Taarifa zaidi baadae.

Takribani saa 11:40as (majira ya Tanzania) Blogu ya Michuzi, http://issamichuzi.blogspot.com inatanabahisha kuwa mabomu yamelipuka...
...Mbagala Kizuiani karibu na kambi ya jeshi,wilaya ya Temake, jijini Dar.
Watoto waliofariki ni Reginal (6) Rajab Said (6), aidha katika mlipuko huo pia kulikukuwepo na majeruhi watatu ambao ni mtoto Sada Seleman (2) Asha Seleman (5) pamoja na Stella Christian Chawala ambaye amejeruhiwa vibaya na kukimbizwa hospitali ya Muhimbili kitengo cha wagonjwa mahututi.

Chanzo cha Mlipuko huo umeshwa na baadhi ya mabaki ya mabomu yaliyokuwa yamebaki,hivyo familia hiyo ilipokuwa inafanya usafi katika nyumba yao na kuchoma moto baadhi ya taka taka, ukapelekea mabaki ya mabomu hayo kulipuka

Aidha Mkuu wa mkoa Mh Lukuvi pamoja na kamanda Kova wameiambia Globu ya jamii kuwa ni kweli tukio hilo limetokea na ni bahati mbaya kwa kilichotokea,hata hivyo taratibu mbambali za tukio hilo zinaendelea kufanyika.