Habari za uchawi: 'Gongagonga' afumwa akimlawiti mume wa mtu

POLISI mkoani Dodoma inamshikilia kijana mmoja wa umri wa miaka 17 kwa tuhuma za kumlawiti mwanamume mwenzake kwa njia za kishirikiana.

Kijana huyo mkazi wa Chali, Isanga aliyejulikana kwa jina la Maneno Ngo’nda na ambaye ni maarufu kama ‘gonga gonga”, alikamatwa majira ya saa 6:00 usuiku kwenye kijiji hicho baada ya kufumwa akifanya kitedo hicho. Kamanda wa polisi mkoani hapa, Zelothe Stephen alisema kijana huyo, ambaye aliwahi kukamatwa kwa tuhuma za kuingilia wake za watu kwa njia za kimazingara, anaonekana kuwa na uzoefu wa kazi hiyo. Kamanda Zelothe alisema kuwa mtuhumiwa alikamatwa na wananchi waliomkuta akimlawiti mwanaume mwenye umri wa miaka 30 (jina limehifadhiwa) wa kijijini hapo. Zelothe alisema tukio hilo lilitokea wakati mtu huyo alipokuwa amelala na mkewe na kwamba mtuhumiwa alimtoa kitandani na kumshusha chini na kumfanyia kitendo hicho. Kwa mujibu wa Zelothe baada ya mke wa mtu huyo kuamka na kumkosa mumewe kitandani aliwasha taa na kumkuta mtuhumiwa akiendelea na kitendo hicho ndipo alipopiga kelele kuomba msaada.

Akihojiwa kuhusu tukio hilo mtuhumiwa alisema kuwa alifanya hivyo baada ya kuona amewamaliza wanawake wote wa kijiji hicho. Alisema anawaingilia kimazingira ya kishirikina bila kujitambua na kufanya nao tendo la ndoa bila wao kujua kitu ambacho alikiri kuwa amekuwa akikifanya mara kwa mara na hivyo wanawake wa hapo kijijini wote aliokuwa akiwapenda alishafanya nao mapenzi. "Nimewamaliza wanawake wote hapa kijijini, sasa naona kuwa imefika zamu ya wanaume na kwamba huyu niliyekamatwa nae alikuwa ndio mwanaume wa kwanza kufanya tendo hili," alisema Gongagonga.

Kamanda huyo alisema katika kesi ya awali mtuhumiwa aliachiwa huru kutokana na kukosekana kwa ushahidi wa kuthibitisha kuwa alimuingilia bila ridhaa mwanamke mmoja kijijini hapo kwa kutumia njia ya kishirikina
Imeripotiwa na Habel Chidawali, Dodoma