Hivi hii nchi ya kizazi cha walawiti na wabakaji ni aje?

Juzi aliripotiwa jamaa 'gonga gonga' wa Dodoma aliyekamatwa kwa kumdunga mwenzie ki'popo-bawa'. Kesho yake, yaani jana, akaripotiwa kijana wa Kinondoni kwa kulawiti kitoto kidogo. Leo anaripotiwa mwingine hapo hapo K'ndoni kwa kubaka. Tizama umri wa wanaohushiwa na matukio haya, wote ni vijana chini ya miaka 21, ndo kusema wameshamaliza shule hawana cha maana cha kuwaza zaidi ya ngono? Ndo kusema elimu waliyopata (kama walikwenda shule) haikuwasaidia kujiajiri? (nani anajali kurekebisha mitaala ya kufundishia) Ndo kukubali usemi 'akili tupu ni karakana ya shetani' (tafsiri ya msemo wa Kiingereza, 'an empty mind is a devil's workshop'). Fikiri nchi ambayo vijana wake ni vibaka na walawiti itakavyokuwa hapo baadaye... halafu tunaendelea kubishana kuhusu maambukizi ya VVU? Tuna laana nawe (ndiyo kisingizio changu) kama si laana kwa nini hali hii?
MSHITAKIWA Issa Juma (20), mkazi wa Kinondoni, amefikishwa katika Mahakama ya Wilaya Kinondoni kujibu shitaka la kubaka. Mbele ya Hakimu Richard Kabate imedaiwa na mwendesha mashitaka Inspekta wa Polisi Boniface Edwin kuwa mshitakiwa alitenda kosa hilo Septemba 16, mwaka huu. Imedaiwa mahakamani hapo kuwa mshitakiwa alimbaka Neema Joshua mwenye umri wa miaka 15 huku akijua na kosa kisheria. Mshitakiwa amekana shitaka hilo na kesi itatajwa tena Oktoba 6, mwaka huu.
Dorothy Meshack, darleo.co.tz  Kinondoni