Nchi moja. Barabara moja. Tofauti hii...

Ama kwa hakika taswira moja yaweza kuwa na maelezo si chini ya elfu moja!
Picha hii inaonesha watu wakiwa katika shughuli zao za kawaida katika maisha, mmoja akipulizwa upepo mwanana wa gharama wa kiyoyozi, il hali huku pembeni ni mwingine akipulizwa kwa upepo mwanana huria wa wote.
Yule anapelekwa ndani ya gari, il hali huyu anapeleka mkokote.
Gharama ya juu imelinganishwa toka kwa mtizamo wa mwenye mkokoteni huenda gharama kwa mtizamo wa mwenye gari ikawa si ya juu hivyo nilivyowaza mie.
Wote ni binadamu na wote wanaishi katika kipande hiki hiki cha ardhi cha dunia tunachokitumia sote.
Wa kale waliposema, 'tajiri na gari yake, maskini na mkokoteni wake', waliona mengi.
Ama kwa hakika binadamu wote ni sawa, ila wapo walio sawa zaidi...

Picha kwa hisani ya gazeti tando la HabariLeo