Pepo la ulawiti linaendelea kuchanua Tanzania

Jana niliposti habari ya kuudhi yenye kichwa cha habari, 'Habari za uchawi: 'Gongagonga' afumwa akimlawiti mume wa mtu" haijapita hata saa 24 tayari kisa kingine cha kufanana na hicho kimeripotiwa Dar. Jiulize ni visa vingapi havijaripotiwa!


MWANAFUNZI wa shule ya Sekondari Mohamed Ramadhani (18), mkazi wa Mpiji amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kinondoni kujibu mashitaka ya kumlawiti mtoto wa kiume.
Mbele ya Hakimu Suzan Kihawa imedaiwa na Mwendesha Mashitaka Inspekta wa Polisi Benedict Nyagabona kuwa, Juni mwaka 2009, mshitakiwa kwa makusudi alimlawiti mtoto wa kiume na kumsababishia maumivu makali sehemu zake za siri. Mshitakiwa amekana mashitaka hayo na kesi hiyo itatajwa tena Septemba 30, mwaka huu.
Wednesday, 23 September 2009 11:52, Rehema Maigala, Kinondoni, http://darleo.co.tz