Upumbavu tu! "Wauguzi na Madaktari watuhumiwa kwa wizi wa dawa"

Watu wasiokuwa na adabu wala lepe la woga ndo wanaweza kufanya mambo kama haya. Kusingizia ati mishahara midogo ndo iwe sababu ya kuonea mwananchi ni sababu ya kipumbavu mno, hata asiyekwenda shule anaitumia hiyo. Badala ya kuonesha utofauti wa akili na maarifa, jitu linatumbukia kufanya anayofanya asiyekwenda shule, ndo maana hata wanasema kama wasomi wanafanya utumbo huu kama sisi, ipo haja gani ya kwenda shule na faida ya kusoma ni ipi? Maarifa-less! Wapumbavu sana tu wote mnaofanya hivi. Ni upumbavu tu, kama wangekuwa na akili wasingefanya hivi kisha wasingizie njaa, upumbavu tu. Kama ni njaa si wende udai haki yako huko inakotakikana? kwani Mwananchi ndo anakunyima haki yako? Upumbavu tu.
WANANCHI wa Kata ya Mzenga wilayani Kisarawe mkoani Pwani wameiomba Idara ya Afya wilayani humo kuwachukulia hatua baadhi ya wauguzi na madaktari wanaojihusisha na wizi wa dawa katika kituo hicho na kuyauza tena kwa walengwa kwa maslahi yao binafsi. Walisema baadhi ya wauguzi na madaktari hao wameanzisha viduka vidogo vya kuuza dawa ambapo huzichukua kituoni hapo na kuziuza katika viduka hivyo. Waliendelea kusema kuwa mgonjwa anapofika kupata matibabu katika kituo hicho, huwa wanakosa dawa, lakini katika viduka hivyo dawa hupatikana, jambo linalowafanya wagonjwa kuwa katika wakati mgumu wa kupata huduma bora za afya.

Akizungumza na waandishi wa habari Kaimu Mganga Mkuu wa Hospitali ya Wilaya, Dk Elly Helela, alikanusha tuhuma hizo na kusema kuwa wauguzi na madaktari katika vituo vya afya, zahanati na hata hospitali ni vigumu kuiba dawa kutokana na vituo hivyo kufanyiwa ukaguzi wa mara kwa mara.

John Gagarini, http://DarLeo.co.tz Kisarawe, Pwani.