Eti huyo mwanamke si angekataa? Na wewe kilichokukataza kukataa kipi hasa? Yeye aweze kukataa na wewe ushindwe una lipi? Hata angekataa, ungekubali? E babu, ukishindwa kutuliza mpira wako mapajani vile vile ujue na mwenzio si malaika aweze kutuliza manyanga yake kiunoni.
Ikiwa mlitenda pamoja na matokeo ya kutenda huko myapokee kwa pamoja. Ikiwa huna imani kama ni mwanao, nenda kapime uhakikishiwe, umzodoe huyo anayekuchongea, lakini usibishe na kuruka kimanga kama juha. Hizi si zama za kuuziwa mbuzi kwenye gunia na kukubali hovyo hovyo tu.
Nimefurahishwa sana matokeo ya kesi hii ambapo aliyekuwa mheshimiwa saaaana mkuu wa Jeshi la Polisi wakati fulani emeamriwa kulipa matunzo kwa mwanae
MAHAKAMA ya Wilaya ya Kinondoni mkoani Dar es Salaam imemuamuru aliyekuwa Mkuu wa Polisi (IGP), Omar Mahita atoe sh 100,000 kila mwezi kuanzia leo kwa ajili ya kumtunza mtoto aliyemtelekeza. Mahakama hiyo pia imemuamuru Mahita alipe malimbikizo ya sh 100,000 kila mwezi tangu alipomtelekeza mtoto huyo, Juma Omar Mahita, mwaka 2003. Habari kamili zinapatikana katika HabariLeo.co.tz na DarLeo.co.tzYaani raha kula, ikifika zamu ya kuosha vyombo haikuhusu, baadaye chombo kikiwa safi watang'ang'ania ni chako. ebo, uwage na soni!