Zoezi la uandikishaji daftari la wapiga kura: Kuku 100 wachomwa moto Pemba

Wameanza kuchoma kuku? inavyoelekea, mwaka ujao kutakuwako na kimbembe cha aina yake. Dalili za mvua ni mawingu... usipoziba ufa, utajajenga ukuta... mchelea mwana kulia, hulia yeye... mzaha mzaha hutumbua usaha... hamna hamna, ndimo mliwamo... samaki mkunje angali mbichi... mzaha mzaha mwishowe hutumbua usaha... lisemwalo lipo ikiwa halipo laja... mwenye macho haambiwi tazama... bora kinga kuliko tiba kamili... ajidhaniaye amesimama aangalie asianguke...
Ni hayo tu kwa sasa!
WATU wasiojulikana wamechoma moto banda la kuku la Katibu Mwenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wa Mkoa wa Kaskazini Pemba, Kombo Hamad Yussuf, zaidi ya kuku 100 wamekufa. Hujuma hiyo inayohusishwa na siasa imefanywa usiku wa manane kuamkia leo katika eneo la Makaani nje kidogo ya kijiji cha Kangagani, jimbo la Ole, Wete. Mkuu wa Wilaya ya Wete, Omar Khamis Othman, amesema leo kuwa, hujuma hiyo imefanywa katika eneo ambalo uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura unaendelea. Amesema, tukio hilo lina uhusiano wa moja kwa moja na mambo ya kisiasa hasa ikizingatiwa kuwa aliyefanyiwa hujuma hiyo ni kiongozi wa CCM.

Kwa mujibu wa Othman, Yussuf amekuwa akiongoza uhamasishaji wa wanachama na wafuasi wa chama hicho kwenda kujiandikisha. “Hii ni siasa moja kwa moja, si ajali ya kawaida… ni jambo la kusononesha mifugo kama kuku haina hatia yoyote inachomwa moto ni masikitiko makubwa sana,” amesema Othman. Kiongozi huyo wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) amesema, Serikali itawasaka wahusika kwa nguvu zote kwa kuwa hujuma hizo zinarudisha nyuma juhudi za kujikwamua na umasikini.

Othman amesema, wanasiasa watabeba lawama kwa kuwa kama si wao hakuna mtu angeweza kuwachoma kuku hao. Amewaomba wananchi watoe ushirikiano kwa Jeshi la Polisi kuwafichua watu wanaofanya hujuma na anaamini ni watu wanaofahamika kwa kuwa hawatoki mbali ya kisiwa cha Pemba. Wakati huo huo kuna taarifa kwamba, watu wasiojulikana wamechoma moto banda la kuku la mfuasi wa Chama cha Wananchi, CUF, Ali Salim Mussa usiku wa kuamkia leo.