Arrogance + Ignorance = ? Mahiza agoma kuwaomba radhi Walimu

You know exactly that YOU ARE DAMN WRONG but you won't admit it ofcourse, why would you? Tell you what, it's a civil thing to do especially for a high figure like you. Guess what, if civility is not a vocabulary to you it could be echoing a form of feeling low in your mind, and that probably doesn't suit you, it belongs to others. I heard you that other day when you opened your mouth, I have it in records (well, ofcourse not that it matters anything to you, but just so you know, I have it in records... just thinking... and wondering... that's all).
But, aren't you the smartest thing ever?
Just listen to yourself...

How does it feel?
Great huh?
What a.......!
One wonders what's the motive and what's behind all that harsh tone!
NAIBU Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Mwantumu Mahiza, amekataa kuwaomba radhi walimu, na amemtaka mwalimu yeyote anayeoona kwamba ualimu haufai au haulipi aache kazi. Mahiza amesema, hafuti kauli hiyo na haombi radhi kwa kuwa alichokisema ni sahihi. “Kuliko mtu kukaa asiwajibike wala kufuata kanuni za kazi na kubangaiza ni bora aondoke ”, amesema Mahiza leo. “Nimesema tena narudia na uandike hivyo hivyo, mimi Mahiza siombi radhi anayeona ualimu haufai au haulipi aanze (aondoke),” amesema.

Rais wa CWT, Gratian Mukoba, leo amemtaka Mahiza afute kauli aliyoitoa Agosti 22, mwaka huu alipozungumza na wanachuo katika Chuo cha Ualimu Songea. Kwa mujibu wa Mukoba, kiongozi huyo wa Serikali aliwataka walimu au wanafunzi wa ualimu wanaoona mshahara wa ualimu ni mdogo kuanzia sasa wakasomee biashara au siasa. Kwa mujibu wa Mukoba, Mahiza aliwataka wenye mtazamo huo waondoke katika taaluma hiyo kwa kuwa haiwafai. “Ni vibaya sana kama mwalimu anafahamu kuwa mshahara ni mdogo halafu anajibaniza hapo, halafu uende ukafanye fujo, wakati umefika shuleni. Kama uko mwaka wa kwanza hujachelewa, hata mwaka wa pili,” Mukoba amemnukuu Mahiza. Mukoba amewaeleza waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Mahiza alitoa msimamo huo baada ya mwanachuo kumuuliza kama Serikali ina mpango wa kuinua viwango vya mishahara. Amemtaka Mahiza awaombe radhi walimu wote nchini kwa madai kuwa, amewadharau na amewadhalilisha. Mukoba amesema, kiongozi huyo amepuuza hadhi ya mwalimu na uhuru wa mwalimu kuhoji, na kwamba, hali hiyo ilitafsiriwa kwamba, walimu wote wanaotaka mishahara mikubwa wamekosea kuchagua taaluma hiyo.

http://habarileo.co.tz/kitaifa