Diego Armando Maradona ashangilia ushindi kihivi...

Ilikuwa ni kiecheko na nderemo kwa timu ya mpira wa miguu ya Argentina baada ya kuichapa Peru bao 2 kwa 1 na hivyo kuibuka mshindi katika mojawapo ya mechi za kinyang'anyiro cha kupata tiketi ya kucheza kombe la dunia litakalofanyika nchini Afrika Kusini hapo mwakani (2010). Kocha wa timu hiyo, Diego Armando Maradona alishindwa kujizuia furaha yake hasa ukizingatia kudorora na kupoteza mechi kadhaa hivyo safari hii alifanya malipizi na kupiga mbizi kiwanjani. Tazama video hapo chini baada ya picha...