Julius Kambarage Nyerere - Mwalimu wewe ni nani? (ushairi)

Nilipo kuwa mdogo niliona picha zako,
Nilipo kwenda shule, tuliimba nyimbo juu yako,
Hata redioni nilisikia ukihutubia,
Vijiweni ulikuwa gumzo,
Mwalimu, wewe ni nani?

Wengine walikuita Mwenyekiti,
Kwa wote ulikuwa ni Rais,
Wengi tunakuita Baba wa Taifa,
Dunia inakujua kama Mwalimu,
Mwalimu, wewe ni nani?

Wajukuu wanakuita Babu,
Watoto wanakuita Baba,
Castrol na Shivji, watakuita Comrade!
Maria anakuita mume,
Mwalimu, wewe ni nani?

Msumbiji na Angola kwao u mkombozi,
Burundi na Rwanda kwao u mpatanishi,
Idi Amini kwake u mvamizi,
Mwalimu, wewe ni nani?

Je Mwalimu wewe ni picha za ukutani?
Au maneno mazuri katika nyimbo na hotuba?
Au ni ile sanamu pale New World Cinema?
Mwalimu, wewe ni nani?

Kama ni Mwenyekiti, Je tu wanachama?
Kama ni Mwalimu, Je tu wanafunzi?
Kama ni Baba wa Taifa Je tu watoto ?
Kwako, Mwalimu ni nani? 

Umendaikwa na Adam Foya, 13.Oktoba.2009
Picha ni mali ya BBC.co.uk