Mdau Eva C anasema 'tule mboga majani tu jamani'

Sisi waTanzania tunafahamu au tumewahi kusikia kuwepo kwa kitoweo 'samaki nchanga', wengine husema 'panya buku' japo watu wengi wanaoishi maeneo ya mjini, neno hili litakuwa la kufikirika tu na pengine mzaha na masikhara. Bila shaka yoyote, nikweli kuwa panya ni kitoweo kwa baadhi ya makabila ya Tanzania hasa yale ya Kusini, mikoa ya Nyanda za juu Kusinina hasa kaskazini kwenye jamii ya Wahadzabe. Vile vile mnyama huyu ni kitoweo katika maeneo ya baadhi ya nchi nyingine za dunia katika mabara kama vile Asia na Amerika ya Kusini.
Baadhi ya viumbe wanaoliwa ambao aghalabu ni nadra kukubalika katika jamii nzima ni pamoja na, Panya, Panya buku, Nyoka, Chura, Ng'e, Mende (aina fulani), Senene, Barale, Kumbikumbi nk.

Hizi ni picha alizonitumia mdau Eva na video inayoonekana hapo baada ya picha nimeipata YouTube.