Ukute Raisi anapika pilau na kudeki chumbani

Ombi langu tukifike huko halafu maraisi wapewe zamu za jikoni na kudeki halafu maji yanakatika, wakachote mferejini kuleee na kuni za kupika hakuna wakakate msituni hukooo kwenye wanyama wakali na wadudu wa kutisha!

Ni ndoto za Alfu Lela U Lela lakini nani anazuia mtu kuota? Nani ataweza zuia mtu kuwaza? tena basi ndoto zenyewe za kulazimishwa, zinatokana na maluweluwe wanayotusababishia wao.

Mi nimetizama hizo picha hapo chini machozi yakanitiririka bila kupenda, halafu nilichokitamka mwenyewe ni siri yangu na moyo wangu na Mungu wangu, na Yeye anajua ni kwa nini nimewaza hivyo.

Halafu nikaendelea tena kuwaza nikajisemea, siku ya kufika huko Mbinguni natamani sana nimkute bibi na babu wote walioteseka wamekalia kiti cha juu kabisa na tayari amekwisha anza kufaidi raha za Mbinguni halafu maraisi wa humu duniani kama akina >|!>|v3I3 na III>|^o|^ hivi wawe tayari wana zamu ya jikoni mmoja kumpikia bibi na babu pilau na mwingine kuwadekia vyumbani mwao.

Ndoto zangu mwenyewe Padri anasema kwenye kitabu imeandikwa, "lisilowezekana kwa Mwanadamu, kwa Mungu linawezekana" yaani ndo kusema hakuna linaloshindikana Kwake, sasa, ombi langu tukifike huko halafu maraisi wapewe zamu za jikoni na kudeki halafu maji yanakatika, wakachote mferejini kuleee na kuni za kupika hakuna wakakate msituni hukooo kwenye wanyama wakali na wadudu wa kutisha!

[gidesign-0034.jpg]
Picha kwa hisani ya blogu ya Mwandandaki Mnyamwezi

[1.bmp]
Picha kwa hisani ya blogu ya Mjengwa Majjid

[gidesign-0045.jpg]
Picha kwa hisani ya blogu ya Mwanandaki Mnyamwezi