Ajinyonga kwa mkanda wa suruali ndani ya Kanisa

Na Shommi Binda, Mara -- MTU mmoja aliyefahamika kwa jina la Salu Geta(50) mkazi wa kijiji cha Masawe mkoani Simiyu amekutwa akiwa amekufa baada ya kujinyonga kwa kutumia mkanda wa Suruali katika kanisa la Anglikana lililopo kijiji cha Serengeti wilayani Bunda mkoani Mara.

Kaimu kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Mara Claud Kanyorota amethibitisha kutokea kwa tukio baada ya kupokea taarifa kutoka kwa wananchi na kwenda
eneo la tukio abapo walimkuta mtu huyo akiwa amejinyonga.

Kanyorota ameitaka jamii kuacha tabia ya kuchukua maamuzi ya kujinyonga na kama kuna kuwa na shida ya yoyote ni vyema kuchukua maamuzi ya kutafuta ushauri kuliko kujinyonga na kupoteza uhai.

Amesema sio vyama kwa mwananchgi kuchukua maamuzi ya kujinyonga hata kama kuna kitu kimemuumiza bali ni vyema kuchukua maamuzi ya kumuona mtu wa karibu yake na kuomba ushauri juu ya kitu ambacho kinamsumbua

Kaimu kamanda huyo wa polisi mkoani Mara ametoa wito kwa wananchi na wakazi wa mkoa wa Mara kwa ujumla kufanya ushirikiano na jeshi hilo kwa kuendelea kutoa taarifa pale kunapoonekana kunaweza kutokea tukio lisilo la kistaarabu.

via blog