Balozi zahimizwa kuutangaza utamaduni wa Tanzania

Msanii wa siku nyingi na mahili wa kucheza na nyoka Bi. Salma Moshi aliongea na Mhe. Balozi Libetara Mulamula alipotembelea Ubalozi wa Tanzania Washington, DC siku ya Jumanne Feb 18, 2014
Msanii wa siku nyingi na mahili wa kucheza na nyoka Bi. Salma Moshi aliongea na Mhe. Balozi Libetara Mulamula alipotembelea Ubalozi wa Tanzania Washington, DC siku ya Jumanne Feb 18, 2014

Wito huo umetolewana msanii wa siku nyingi wa kucheza na nyoka Mama Salima Moshi alipokwenda kumuona Mhe. Balozi wa Tanzania nchini Marekani na Mexico, Mama Mulamula.

Mama Salima alisema Balozi zina nafasi nzuri za kuutangaza utamaduni wetu kwani zipo karibu zaidi na nchi husika. 

Aliomba Baraza la Sanaa Tanzania liandae kitabu kitakachojumuisha wasanii mbalimbali na anwani zao kisha vitabu hivyo vipelekwe kwenye balozi zetu ili watu mbalimbali wanaozuru ofisi hizowaweze kuvisoma na kupata anwani za kuwaalika wasanii watakaoweza kuutangaza utamaduni wetu hali wasanii hao wakijipatia kipato na kujifunza. 

Mama Salima alisema pia mapromota wengi wamekuwa wakiwatelekeza wasanii baada ya malipo na huishia kuwapeleka kuburudisha Watanzania pekee waishio Ughaibuni. Akapendekeza kwua ni wakati umefika wasanii wanaosafiri nje wapate nafasi ya kuburudisha watu wa taifa zima na siyo Watanzania tu. Alitoa mfano kuwa haiwezekani kumwona mwanamuziki wa Marekani kama JayZ amekwenda Tanzania na aishie kuwaburudisha Wamarekani waishio Tanzania tu. 

Mama Salima alikemea vikali swala la kunakili kazi za sanaa kwani linarudisha nyuma maendeleo ya wasanii. Aliomba SERIKALI kutoa adhabu kali kwa watakaobainika. 

Pia aliomba isimamie suala la haki miliki. Alisema imefika wakati sasa wasanii kuwa na Wanasheria ili isaidie kulinda haki zao.

Mama Salima alimshuru sana Mhe. Rais Kikwete ambaye amekuwa wakati wote karibu na wasanii kama ambavyo hivi karibuni aliwaalika kwenye chakula.

Kuhusu tuzo, alishauri ziwe zinatolewa kwa wasanii wa sanaa za maonesho pia. Alisema wakati umefika wa kutoa kibali kwa waandaaji wengine kwani si vibaya zikawa zaidi ya moja. Aliomba pia kusaidiwa kujenga maktaba kwenye eneo la viwanja vya wasanii Mkuranga.

Mhe. Balozi Mulamula alimshukuru msanii huyo na kumpongeza kwa kazi nzuri ya kuwakilisha nchi na kuwa msanii atakayekuwa mfano kwa wengine. Alisema Serikali imejizatiti kikamilifu kuhakikisha haki za msanii zinalindwa. Aliwasihi wasanii kujua haki zao. Aliwasifu wasanii mbalimbali wanaoitangaza Tanzania.

Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tamzania nchini Marekani, Mhe. Liberata Mulamula akimsikiliza msanii wa siku nyingi, Bi Salma Moshi (hayupo pichani) alipotembelea Ubalozi wa Tanzania Washington, DC siku ya Jumanne Feb 18, 2014.

Afisa Mgendi Nzowa akiwa kwenye mkutano huo.
Afisa Mgendi Nzowa akiwa kwenye mkutano huo.

Afisa Suleiman Saleh akijumuika pamoja na Balozi kwenye mkutano huo.
Afisa Suleiman Saleh akijumuika pamoja na Balozi kwenye mkutano huo.
Msanii aliyetamba enzi hizo kwa umahili wake wa kuchea na nyoka Salma Moshi akisalimiana na kumkabidhi picha za baadhi ya kazi ya sanaa hiyo aliyofanya enzi hizo Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Marekani Mhe. Liberata Mulamula alipokwenda kujitambulisha rasmi kwenye Ubalozini wa Tanzania uliopo Washington, DC siku ya Jumanne Feb 18, 2014.