Baraza la Vyama vya Siasa hlijajipanga kuwania Uenyekiti Bunge la Katiba

Mwenyekiti wa Baraza la Vyama vya Siasa Tanzania, Peter Kuga Mziray, alipoulizwa na gazeti la NIPASHE kama vyama vya upinzani vimeweka mkakati wowote wa kumpata Menyekiti wa Bunge hilo, alisema hakuna:
“Kimsingi hakuna mkakati wowote uliowekwa na wapinzami katika kuwania nafasi hiyo, ninachokiona ni kwamba wagombea urais wanaweza kujipenyeza katika suala hili/”
Mziray ambaye ni Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha APPT Maendeleo, alisema mashaka yaliyopo ni kwamba makundi ya urais 2015 yaliopo ndani ya CCM ni lazima yanaweza kujipenyeza katika mchuano wa nafasi ya Mwenyekiti wa Bunge la Katiba.