Binti huyu anomba umsaidie alipe ada 450,000/- ya mwaka wa mwisho wa masomo


Jeni Mkondy 31 Mkaazi wa Luwawasi Kata ya Lizaboni wilaya ya Songea Mkoani Ruvuma anaomba msaada wa kujiendeleza kielimu.

Jeni Mkondy ni mwanamke mwenye umri wa miaka 31. Alibahatika kupata Elimu ya Msingi mpaka darasa la saba. Baada ya kumaliza Elimu ya Msingi aliolewa hakuweza kuendelea na masomo ya Elimu ya Sekondari kutokana na uwezo mdogo.

Aliolewa. Baada ya ndoa alibahatika kupata watoto watatu ambao mmoja yupo kidato cha pili, wa pili darasa la saba na mwingine yupo darasa la kwanza.

Baada ya kutelekezwa na mumewe, aliamua kujiendeleza kielimu. Mwaka 2011 alianza masomo ya kidato
cha kwanza katika sekondari ya St Agaton ambapo aliweza kujilipia ada ya shilingi laki nne (400,000/=) kwa mwaka, kwa miaka mitatu. Kwa sasa yuko kidato cha nne ila amekwama kulipa ada ya mwaka ya shule na ada ya mtihani.
Hivyo, anaomba watu wamsaidie kumlipa shilingi 50,000/= kwa ajili ya ada ya mtihani na shilingi 400,000/= kwa ajili ya ada ya mwaka ya Shule ya Sent Agaton, Songea.

Mwisho wa kulipa ada ya mtihani ni tarehe 28.2.2014, akichelewa, atalazimika kulipa zaidi (limbikizo).

Mawasiliano yake ni: 0716 614405, au 0755 061588.

Pia, ukitaka taarifa zaidi unaweza kuwasiliana na kituo cha Radio Free Afrika, Songea kwa simu namba: 0755 731234.