Bunge la Katiba: Spika ateua 6 kuchunguza malalamiko ya posho za Wajumbe

Mwenyekiti wa muda wa Bunge Maalum la Katiba, Ameir Pandu Kificho, ametangaza majina ya watu sita watakaounda timu kwa ajili ya kuyafanya bora malalamiko yaliyotolewa na baadhi ya wajumbe wa Bugne hilo kuwa ya posho ya Shilingi 300,000/= kwa siku haitoshi kuwawezesha kuifanya kazi hiyo kwa makini.

Akitangaza majina hayo kabla ya kuanza kwa semina kwa wajumbe hao, Kificho alirejea Sheria ya Mabadiliko ya Bunge la Katiba Sura ya 83 toleo la mwaka 2014 na kusema:
“Kuhusu suala la kumudu kuishi vizuri na hii kazi nzito tuliyonayo bado halina majibu kwa sasa” 
Kificho aliyataja majina ya wanaounda tume hiyo kuwa ni:-
  1. William Lukuvi
  2. Mohammed Aboud Mohammed
  3. Freeman Mbowe 
  4. Paul Kimiti 
  5. Asha Bakari Makame
  6. Jenista Mhagama.
Alisema timu hiyo itakutana mara baada ya semina hiyo leo na ikiongozwa na Mwenyekiti huyo wa muda ili kuweza kukaa pamoja na kupanga ya kuweza kuiomba Serikali kuangalia jambo hilo na kuweza kupata majibu.

Timu hiyo imeundwa baada ya baadhi ya wajumbe wa bunge hilo kulalamikia posho hizo ndani na nje ya ukumbi wa Bunge jana.

Nukuu kuhusu malalamiko hayo unaweza kuzisoma kwenye magazeti ya: