Wanamuziki wa Extra Bongo pamoja na Hamis Mwinjuma kwenye ukumbi wa hoteli ya Atriums iliyopo Afrika Sana, Sinza. |
Na Andrew Carlos, GPL — H
AYAWI hayawi, sasa yamekuwa! Ule uzinduzi wa albamu ya ‘Mtendwa Akitendewa’ kutoka bendi ya Extra Bongo kesho utafikia kilele ambapo watadondosha bonge la shoo katika ukumbi wa Dar Live, Mbagala-Zakhem.
Akizungumzia maandalizi ya mwisho kuelekea shoo ya albamu hiyo katika hoteli maarufu ya Atriums iliyoko Afrika Sana, Sinza, jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Extra Bongo, Ally Choky, alisema kila kitu kinaenda sawa na hivi sasa kilichobaki ni kudondosha mashambulizi siku ya kesho usiku.
Burudani hiyo itanoga zaidi kutokana na kusindikizwa na wakali wa Bongo Fleva kina Amin na Linah, Makhirikhiri wa Bongo, Bendi ya Mashujaa, TOT Band chini ya ‘Malkia wa Mipasho’ Khadija Kopa.
Kiingilio kitakuwa ni sh. 6,000 tu.