Jamii Production audio: Kwa nini Facebook imetumia dola bilioni 19 kununua WhatsApp?

Photo: Mobile88.com


Kama wewe ni mmoja wa wanaotumia njia ya mawasiliano iliyojipatia umaarufu ya

WhatsApp, basi ujue kuwa nawe ni miongoni mwa wateja takribani nusu bilioni walioufanya mtandao huo kuwa maarufu zaidi duniani kwa kipindi kifupi tu.

Ni umaarufu huu uliofanya kampuni kubwa ya mawasiliano ya Facebook wiki hii kuona umuhimu wa kutumia dola za kimarekani bilioni 19 kununua WhatsApp.

Lakini kwanini kampuni itumie kiasi hicho kikubwa kwa kampuni kama hii?Hii ni sehemu ya ripoti ya Jamii Production kwenye kipindi cha DAKIKA 90 ZA DUNIA kinachorushwa na kituo cha Radio cha Capital FM cha Dar Es Salaam Tanzania kila Jumamosi kuanzia saa moja na nusu asubuhi (7:30 AM).

Hii ilikuwa ripoti ya Februari 22, 2014