Mafunzo ya bure ya Ualimu wa Ujasiriamali

Taasisi ya RAFIKIELIMU FOUNDATION kupitia mradi wa ELIMU YA UJASIRIAMALI MIJINI NA VIJIJINI, inatangaza nafasi za MAFUNZO YA UALIMU WA UJASIRIAMALI.

Wahitimu wa mafunzo haya watapata nafasi ya kufanya kazi kwa kujitolea kama waalimu wa ujasiriamali katika MRADI WA ELIMU YA UJASIRIAMALI MIJINI na VIJIJINI.

IDADI YA NAFASI :

Nafasi 5 katika kila kata ya jiji la Dar Es salaam.

SIFA ZA MWOMBAJI :-
  1. Awe raia wa Tanzania mwenye elimu ya kuanzia kidato cha nne na kuendelea.
  2. Awe mkaazi wa Dar es salaam.
  3. Awe na wito wa kufanya kazi ya ufundishaji.
  4. Awe tayari kufanya kazi kwa kujitolea kama mwalimu wa ujasiriamali katika kata yoyote ya jiji la Dar es salaam.
MAFUNZO yatatolewa kwa mwezi mmoja kuanzia tarehe 10 Machi 2014 katika Chuo Chetu kilichopo katika eneo la Changanyikeni.

ADA YA MAFUNZO: Mafunzo haya yatatolewa bila malipo yoyote, yaani BURE.

Chuo chetu kinapatikana katika eneo la Changanyikeni karibu na Chuo cha Takwimu mbele ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

JINSI YA KUTUMA MAOMBI : Matumbi yote yatumwe kupitia barua pepe yetu ambayo ni :[email protected]

MWISHO WA KUCHUKUA FOMU ZA MAOMBI NI TAREHE 28 FEBRUARI 2014.