Makamu wa Rais, Dkt Bila awasili Mwanza kwa kongamano la uwekezaji Kanda ya Ziwa

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal akishuka kwenye ndege wakati alipowasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Mwanza jioni ya leo, tayari kwa ufunguzi Kongamano la uwekezaji kwa Kanda ya Ziwa, linaotarajiwa kuanza kesho kwenye Hoteli ya Malaika jijini Mwanza.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Bilal akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza,Mh. Everist Ndikilo wakati alipowasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Mwanza jioni ya leo.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Bilal akisalimiana na Naibu Waziri wa Madini, Mh. Charles Kitwanga.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Bilal akisalimiana na Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji nchini (TIC) ambao ndio waratibu wa Kongamano hilo,Bi. Julieth Kairuki,wakati wakati alipowasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Mwanza jioni ya leo.Makamu wa Rais yupo jijini Mwanza kwa ajili ya Ufunguzi wa Kongamano la Uwekezaji kwa Kanda ya Ziwa,linalotarajiwa kuanza kesho kwenye Hoteli ya Malaika,jijini humo. 

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mh. Everist Ndikilo (kulia) akizungumza jambo na Mkuu wa Mkoa wa Kagera,Kanali Mstaafu Fabian Massawe wakati walipotembelea hoteli ya Malaika kukagua maendeleo ya Maandalizi ya Kongamano hilo litakalofunguliwa na Makamu wa Rais, Dkt. Bilal. Katikati ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji nchini (TIC) ambao ndio waratibu wa Kongamano hilo,Bi. Julieth Kairuki