MATOKEO YA TATHMINI YA MCHAKATO WA UHAMAJI KUTOKA MFUMO WA UTANAGAZAJI WA ANALOJIA KWENDA KIDIJITI
Jopo hilo lilijumuisha wataalamu wafuatao:-
Dr.Francis Sichona Mtaalamu wa Takwimu
Mr.F.M Ishengoma Mtaalamu wa Habari na Mawasiliano
- Madhumuni ya tahmini hii ilikuwa imejengwa kwenye maeneo Makuu manne kama ifuatavyo;
- Tathmini ya utendaji na utoaji huduma za utangazaji kwenye mfumo wa kidijiti ikiwa ni pamoja na usimikaji wa miundo mbinu ya kidijiti.
- Tathmini ya kuangalia jinsi Mamlaka ya Mawasiliano ilivyokuwa imejizatiti kuandaa na kusimamia zoezi zima la uhamaji toka mfumo wa utangazaji wa analojia kwenda kidijiti
- Tathmini ya jinsi watumiaji wa huduma za utangazaji walivyopokea mabadiliko hayo na changamoto zilizopo na
- Tathmini ya jinsi zoezi zima la uzimaji mitambo lilivyoendeshwa.
(ii) Idadi ya watu walioweza kununua visimbuzi ilikuwa ndogo hivyo watu wengi kushindwa kununua na kukosa habari zinazopatikana kwa njia ya luninga,
(iii) Ushirikishaji wa wadau kwenye mchakato mzima wa uhamaji toka mfumo wa analojia kwenda kidijiti kabla ya uzimaji mitambo hiyo,
(iv) Kiwango cha Elimu kwa Umma (Public Awareness Campaign) kilichotolewa kabla na baada ya uzimaji mitambo,
(v) Bei za visimbuzi kama zilikuwa juu kwa watu wa hali ya kawaida na kusababisha kushindwa kuvinunua,
(vi) Ubora wa visimbuzi na upokeaji wa matangazo usioridhisha kama vile kuganda kwa picha.
(iii) Wasimikaji wa miundo mbinu ya kidijiti (Multiplex Operators) na
(iv) Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania.
- 5.5% hawakununua visimbuizi
- 0.1% ya Kaya, walisema visimbuzi vilikuwa havipatikani
- 3.2% ya Kaya, walishindwa kunua visimbuzi sababu ya bei kuwa juu
- 0.2% ya Kaya visimbuzi vyao vilikuwa vibovu
- 0.3% ya Kaya, visimbuzi havikuweza kupokea matangazo ya kidijiti kwa sababu ya mawimbi hayapatikani kwa ubora zaidi (Poor signal reception)
- 0.9% ya Kaya Luninga (TV screen) zilikuwa mbovu
- 0.7% ya Kaya hawakuwa na umeme
2.2 UTAYARI WA MAMLAKA YA MAWASILIANO KUANDAA NA KUSIMAMIA ZOEZI ZIMA LA UHAMAJI TOKA UTANGAZAJI WA MFUMO WA ANALOJIA KWENDA KIDIJITI
- Muundo bora wa leseni unaozingatia utoaji huduma za matangazo ya kidijiti,
- Utaratibu mzuri wa ushindani kwa njia ya wazi uliotumika kuwapata “Multiplex Operators” (wajenga Miundombinu na Wsambazaji wa matangazo),
- Waraka unaonyesha mchakato wa namna ya kupata malipo yananayotakiwa kulipwa na watengenezaji na wasambazaji wa maudhui (Transmission fee) kwa wenye leseni ya miundo mbinu ya kidijiti (Multiplex Operators),
Tathmini imeonyesha kuwa kati ya kaya zote zilizohojiwa kwenye miji saba, ni 0.1% ya kaya zilizodai uhaba wa visimbuzi wakati wa zoezi zima la uzimaji mitambo ya analojia. Matokeo mingine ni kama ifuatavyo:-
- 35.4% ya kaya zilizohojiwa walinunua visimbuzi kabla ya uzimaji mitambo ya analojia na kabla ya kuanza utoaji wa elimu kwa umma kuhusu mfumo mpya wa uatangazaji wa kidijiti
- 29.5% ya kaya walinunua visimbuzi kabla ya uzimaji mitambo ya analojia lakini baada ya utoaji elimu kwa umma
- 35.1% walinunua visimbuzi baada ya uzimaji mitambo
2.5 WATENGENEZAJI NA WASAMBAZAJI MAUDHUI (CONTENT SERVICE PROVIDERS)
3.0 MAJUMUISHO
Prof. Nerey Mvungi - Mtaalamu wa Mawasiliano ya ki electronic
Dr.Francis Sichona - Mtaalamu wa Takwimu
Mr.F.M Ishengoma - Mtaalamu wa Habari na Mawasiliano
19 FEBRUARI 2014